Mtoto
akiangalia bila woga Kakakuona aliyepatikana nyuma ya nyumba ya Tatu Katala,
Mtaa mpya wa Chaboko, Kigamboni Dar es Salaam jana. Mnyama huyo ambaye kuonekana
kwake ni nadra inadaiwa ana uwezo wa kutabiri matukio mbalimbali yanayoweza
kutokea siku za usoni. Kwa mujibu wa mtoa maelezo ya utabiri huo, Nadhiru Ali
alisema siku zijazo nchi itakumbwa na vurugu lakini siyo vita, baada ya mnyama
huyo kugusa sarafu, unga na kunywa maji.
Mama mwenye nyumba akizungumza na maafisaa mali asili
Mwananchi akimwangalia Kakakuona kwa ukaribu zaidi
wananchi wakiangalia Kakakuona baada ya kuchukuliwa kwa gari
Mpigapicha wa gazeti la Jambo Leo, Khamis Mussa akimshika Kakakuona ili
apate neema na baraka Kakakuona
MNYAMA Kakakuona ameonekana Kigamboni, Dar es Salaam, ambapo
pamoja na mambo mengine ametabiri mwakani kutokea vurugu lakini si vita.
Utabiri huo umekuja siku moja baada ya Mtoto wa aliyekuwa Mtabiri Mashuri
Afrika Mashariki na Kati, Sheikh Yahya Hussein(marehemu), Alhaji Maalim Hassan
Hussein naye kutabiri kutokea vurugu mwakani.
Kakakuona huyo aliyeonekana nyuma ya nyumba ya Tatu Katala, Mtaa mpya wa Chaboko, Kata ya Vijibweni, Kigamboni Dar es Salaam, aligusa sarafu, unga, kunywa maji na kutikisa mkia ambao ishara yake ni kuwepo vurugu mwakani. Kwa mujibu wa mtoa maelezo ya utabiri wa mnyama huo, Nadhiru Ali ni kwamba, kugusa kwake sarafu ni ishara njema ya uchumi, unga ni neema ya chakula na maji ni kuwepo kwa mafuriko.
Akisimulia kuhusu tukio hilo, mama mwenye nyumba, Katala, alisema kuwa alistuka usiku baada ya kusikia miguno ya mbwa na kuku ndipo aliamka na kwenda nyuma ya nyumba yake na kushangaa kuona kitu chenye magamba kama Kenge.
Alisema baada ya watu kukusanyika ndipo baadhi yao wakagundua kuwa ni Kakakuona na kuanza kumuwekea vitu mbalimbali ili atabiri. Baadhi ya vitu waliomuwekea ni fedha, maji, tofali, kisu, unga, mchele na fimbo.
Kakakuona aligusa, sarafu, unga, fimbo na kunywa maji na kuacha vitu vingine. Tukio hilo lilikusanya watu wengi waliokuwa na hamu ya kutaka kumgusa ili wapate neema na baraka. Baadaye walitokea maofisa wa Maliasili na kumchukua mnyama huyo kwa ajili ya kwenda kumhifadhi.
Chapisha Maoni