Mwanamke
mmoja anasakwa na polisi Kabete baada ya kudaiwa kumchoma mumewe kwa maji ya
sima na kisha kumficha nyumbani siku tano katika kijiji cha Muthure, eneo bunge la Kabete.
Mwanamume huyo sasa anauguza majeraha hospitali
Mwanaume
huyo aliokolewa na majirani baada ya
siku tano za kufichwa na mkewe aliyemchoma kwa maji moto kwenye kichwa na kifua
katika kijiji hicho,
Majirani walishangaa walipomkosa Bw
Samuel Mungai, mwanamume waliyemjua kama mcheshi na aliyependa kileo chake na
ndipo wakaanza kumsaka.
Chifu wa
eneo hilo Peter Njoroge alisema kuwa wanakijiji walimpata Bw Mungai huku amefungiwa
katika nyumba yake na majeraha mabaya, ambayo yalikuwa yameanza kunuka,
yaliyosababishwa na maji moto.
“Lilikuwa
jambo la kusikitisha kupata mwanaume huyu amechomeka vibaya sana kwenye kifua
na kichwa,” alisema Chifu Njoroge.
Mwanaume
huyo, Bw Mungai alihadithia yaliyomsibu kabla ya wenyeji kumpeleka katika kituo
cha polisi cha Kikuyu kuandikisha ripoti ya uhalifu wa kinyama aliofanyiwa na
mkewe, Joyce Wakanyi. Ripoti kwa
polisi ilisema kuwa, siku ya Jumamosi, mwanaume huyo alifika nyumbani kama
kawaida na kupata mkewe nyumbani. Shida ilizuka nyumbani wakati Bi Wakanyi
aliuliza mwanaume huyo, ambaye anafanya kazi ya useremala kama alikuwa na
kiwango fulani cha pesa ambacho alihitaji. La
kushangaza ni kuwa, bwana huyu alisema kuwa hakuwa na pesa hizo, Sh1,000,
ambazo mkewe alihitaji, lakini alikuwa amelewa, hali ambayo majirani
walithibitisha kuwa anapenda kunywa pombe sana.
Kwa hasira,
inadaiwa baadaye mkewe alichukua maji yaliyokuwa kwenye jiko ya kupikia sima na
kumwagia mumewe aliyekuwa amelala.
Wawili hawa, Bw Mungai na Bi Wakanyi wameishi kama mume na mke kwa zaidi ya miaka 18 na wako na watoto wanne.
Wanakijiji
walifanya mchango wa harambee na kupeleka mwanaume huyo hadi Hospitali ya
Wilaya ya Tigoni ambako anaendelea kupata matibabu.
Chifu
Njoroge alisema kuwa si mara ya kwanza mwanamke huyo kumdhuru mumewe.
“Kuna wakati
alimchapa na kumvunja mguu na mara nyingine kumuumiza mbavu,” alisema.
“Nina
hofu kuwa suluhu isipopatikana kukomesha ugomvi katika boma hili, watapata
kuuana,” aliongeza Chifu Njoroge.
Mwanamke
huyo, Bi Wakanyi, anasakwa na polisi baada ya kutoroka na kuacha watoto wake
nyumbani huko Muthure.
Duh! hatari kweli kweli
Chapisha Maoni