Timu ya Taifa ya Soka ya Uganda, leo imeilaza Liberia
kwa bao moja kwa bila na kuimarisha matumaini yake ya kufuzu kwa kombe
la dunia mwaka ujao nchini Brazil, katika mechi kali iliyochezwa mjini
Kampala.
Kufuatia ushindi huo Uganda Cranes sasa imepanda
hadi nafasi ya pili katika kundi J na alama 5 nyuma ya vinara wa kundi
hilo Senegal ambao wanachuana na Angola. Uganda sasa imesalia na mechi mechi mbili na
imepangiwa kuchuana na Angola tarehe kumi na tano mwezi huu kabla ya
kupepetana na Senegal tarehe 6 Septemba mwaka huu katika uwanja wa
Leopold Senghor.
Uganda ni sharti ishindi mechi zake zilizosalia
ili kuwa katika nafasi nzuri ya kufuzu kwa fainali hizo zitakazoandaliwa
nchini Brazil Januari mwakani. Katika mechi zingine za kufuzu kwa Fainali hizo,
Zambia wameilaza Lesotho kwa magoli manne mwa yai nayo Botswana
wakalemewe nyumbani kwao na Ethiopia kwa kufungwa magoli mawili kwa
moja.

Chapisha Maoni