Harambee Stars imeondolewa kwenye
kinyang'anyiro cha kufuzu kombe la dunia 2014
Mchuano wa kufa na kupona
ulishuhudiwa kati ya bingwa wa Afrika Super Eagles wa Nigeria na Harambee Stars
wa Kenya katika uwanja wa kimataifa wa Moi Kasarani mjini Nairobi. Musa Ahmed aifungia Nigeria bao la kwanza
na la pekee kunako dakika ya 81. Mashabiki wa Kenya Kimya!
Baadhi ya mashabiki wa timu ya taifa
ya Kenya Harambee Stars waanza kuondoka uwanjani.
Mashabiki wa Nigeria hawakuwa wengi
uwanjani wakikisiwa kufika 300, lakini licha ya uchache wao ,hawakufa
moyo.Mandishi wa BBC Odeo Sirari aliyekuwa uwanjani,alishuhudia mashabiki
wachache wa Nigeria wakiisiahngilia timu yao kwa nyimbo na ngoma japo hawakuwa
wanasikika kutokana na mayowe ya wakenya. Ilikuwa mechi ya mkondo wa pili kwa
timu hizo mbili baada ya kwenda sare ya bao moja kwa moja walipocheza kwa
mkondo wa kwanza mjini Calabar Nigeria mwezi jana.
Mechi hii ni ya kundi la F ya
kugombania nafasi ya kushiriki michuano ya kombe la Dunia mwakani nchini
Brazil. Vijana wa kocha Stephen Keshi,
wanatarajiwa kuendeleza ushindi wao hii leo wakijitafutia nafasi ya kuwakilisha
Afrika katika michauno ya kombe la dunia nchini Brazil Kwa vijana wa Eagles wanaosemekana
kujiandaa vyema, wanafahamu kuwa ikiwa watashindwa basi itakuwa hasara kwao
kwani hawataweza kwenda Brazil.
Licha ya kwenda sare mwezi jana,
Nigeria inaingia kwenye mkondo huu bila ya kushindwa mechi yoyote ya makundi
kati ya kumi na sita zilizocheza hadi kufikia sasa.
Wadadisi wanasema Eagles wanaonekana
kuwa katika nafasi nzuri ya kushinda. Mwandishi wetu Odeo Sirari alipiga kambi
katika uwanja wa Moi Kasarani kutupasha mambo yalivyokuwa.
14:50 PM :Shamra shamra zimeanza
kupamba moto katika uwanja wa kimataifa wa Moi Kasarani. Mwandishi wa BBC
ambaye yuko katika uwanja huo Odeo Sirari, anasema kuw mashabiki wanzidi
kumiminika uwanjani. Milango ya uwanja ilifunguliwa rasmi majira ya saa tano
asubuhi
14:58 PM: Mojawapo ya mabango ya
mashabiki uwanjani yana bendera ya Kenya na maandishi ''Oga you are finished''
kwa maana kuwa Nigeria itashindwa . Odeo anasema hayo ni maoni ya mashabiki wa
Nigeria uwanjani
Timu zote zina mbili zina uhakika
zitashinda mechi ya leo. Tuache tuone msema kweli
Mechi inatarajiwa kuanza saa kumi
kamili. Rais Uhuru Kenyatta anatarajiwa kuhudhuria
15:43 PM: Mashabiki washangilia
wachezaji wa Harambe Starrs wakiingia uwanjani. Super Eagles nao pia wameingia
uwanjani . Wachezaji wa pande zote mbili sasa wanapasha misuli joto
15:48 PM: Uwanja wa michezo wa Moi
Kasarani una uwezo wa kushenei mashabiki takriban 60,000
15:49 PM: Kikosi cha Harambe Stars:
Mlinda lango Duncan Ocheng, Safu ya ulinzi David Owino Brian Mandela David
Ochieng . Wachezaji wa kiungo cha kati Mulinge Ndeto, Victor Wanyama Jamal
Mohammed,Johana Omolo na Peter Opiyo. Washambulizi ni Kefa Aswani na Fracis
Kahata
16:07 PM: Mechi imeng'oa nanga rasmi
. Kikosi cha Eagles...Efe, Oboabona, Omeroo Elderson, Onazi, Mikel, Mba,Oduamadi,Musa,
Ideye Golikipa ni Enyeama
16:33 PM baada ya mechi kuchezwa kwa
zaidi ya dakika thelathini bado timu hizo ziko sare tasa
16:41 Mshambuliaji wa Kenya Kepha
Aswani anenekana akichechema uwanjani na kuwa mashabiki wanataka aondolewe
16:51 Shambulizi katika eneo la
hatari lango la timu ya Kenya. Sunday Mba aliupiga mpira kwa kichwa lakini
ukapaa juu ya mlingoti wa goli . Mashabiki wa Kenya wabaki kimya
17:27 pm Peter Opiyp atekeleza
shambulizi lango la Nigeria.
17:28 Nigeria yafanya mabadiliko,
SundayMba aondolewa
17:28 Victor Wanyama apata
jeraha..anahudumiwa. Kenya yashambulia, Kombora la Johhana Ngeno lapaa juu ya
mlingoti kunako dakika ya 56. Victor Wanyama arejea uwanjani, mashabiki wa
kenya washangilia. Nigeria inahitaji ushindi katika mechi hii dhidi ya Kenya
ili kusonga mbele. Sare ya kutofungana itaipa Kenya nafasi nzuri ya kusonga
mbele
17:38 pm: Mlinzi wa kati wa Harambee
Stars Brian Mandela afanya kazi ya ziada kupangua makombora ya wa Nigeria.
Mashabiki wa Kenya wanaimba: '' Haki
yetu! Bao! Haki yetu! bao!
Victor wanyama aondoka tena
uwanjani, yamkini jeraha lake ni baya.
Timu ya taifa ya Nigeria yafanya
mabadiliko dakika ya 64 anaondoka Brown Aye anaingia Ujah Antony
17:39 pm: Victor Wanyama arejea tena
uwanjani licha ya kuonekana amejeruhiwa. Mashabiki wa Kenya wanataka aendelee
kucheza.
17:40 Mulinge Munandi aonyeshwe kadi
ya njano kwa kumfanyia masihara mchezaji wa Nigeria Musa Ahmed. Harambee stars
yazidisha shinikizo dhidi ya Super Eagles. Mashabiki wakosa subira.. wanaimba
haki yetu! bao! haki yetu! bao.....
Peter Opiyo wa harambee stars
aondolewa, Patrick Osiako aingia uwanjani.
17:52 pm: Mashabiki wa timu ya taifa
ya Nigeria kama mia 200 hivi washangilia bao lililofungwa na Musa Ahmed. Baadhi
ya mashabiki wa Kenya wawazomea wenzao wa Nigeria kwa kuwarushia chupa za maji.
Safu ya mashambulizi ya Harambee
stars yaonekana kufifia.
Dakika ya 87, Oduamani wa Nigeria
aondoka anaingia Ogude.
Nigeria yapata kona ya pili kipindi
cha lala salama.

Chapisha Maoni