UFAHAMU MMEA WA MLONGE NA NAMNA UNAVYOFANYA KAZI NDANI YA MWILI WA MWANADAMU



Image result for mlonge
Mlonge au Moringa oleifera kwa kiingereza umekuwa ukijulikana kama mti wa miujiza kwa karne nyingi katika baadhi ya nchi za Afrika, Asia na katika nchi za Caribbean. Mti huu umeripotiwa kutibu zaidi ya magonjwa 300 ikiwemo magonjwa mbalimbali sugu.
Karibu kila sehemu ya mti huu hutumika kama dawa. Majani ya mlonge yanaweza kutafunwa mabichi, yaliyochemshwa kama mboga au yaliyokaushwa na kusagwa kuwa unga. Unga wa mlonge unaweza kuhifadhiwa kwa miezi kadhaa bila kupoteza ubora na faida zake za kiafya.
Mbegu za mlonge zimekuwa dili kubwa duniani kwa sasa, zinahitajika kwa kiasi kikubwa katika nchi ya Marekani na China na kwa mjibu wa taarifa ni kuwa zinauzwa mpaka shilingi 45000 ya Tanzania kwa gramu 500. Walikuja pia wachina kuzinunua kwa wingi na walipokuwepo hapa Tanzania bei ya mbegu za mlonge ilifika mpaka 11000 kwa kg kwa bei ya jumla yaani kwa anayechukua kg 100 au 500 au 1000 na kwenda juu. Taarifa zisizo rasmi zinadai Wachina hawa walikimbia nchini baada ya serikali kuanza kufuatilia na kuwakamata wakwepaji kodi bandarini. Isingekuwa hivi mpaka leo mlonge ungekuwa umeshatoweka wote Tanzania.
Faida za mlonge zimeandikwa na majarida ya afya na lishe kadhaa duniani. Kile ulikuwa hujui ni kuwa viwanda na makampuni mengi ya dawa za hospitalini yamekuwa yakitumia virutubishi vilivyomo kwenye mti huu kutengenezea madawa kwa ajili ya binadamu na wanyama.

MLONGE UNA MAMBO MBALIMBALI AMBAYO YANAFAIDA NYINGI NDANI YA MWILI WA MWANADAMU
*Kalsiamu mara 17 zaidi ya ile ya maziwa ya ng’ombe
*Potasiamu mara 15 zaidi ya ile ya kwenye ndizi
*Una vitamini A mara 10 zaidi ya ile ya kwenye karoti
*Una protini nyingi mara 9 zaidi ya ile ya kwenye mtindi (Yogurt)
*Una Klorofili (kemikali ya rangi ya kijani ipatikanayo katika mimea) mara 4 zaidi ya ile ya kwenye nyasi au majani ya ngano (wheatgrass)
*Una madini chuma (iron) mara 25 zaidi ya yale ya kwenye Spinach
*Una vitamini A mpaka Z,
*Una Omega 3, 6, na 9
*Una asidi amino zile mhimu zaidi zinazohitajika na mwili
*Una kiasi cha kutosha cha madini ya Zinc ambayo ni madini mhimu katika kuongeza homoni za kiume na nguvu za kiume kwa ujumla

MLONGE NDICHO CHAKULA CHENYE AFYA ZAIDI KULIKO CHAKULA KINGINE CHOCHOTE JUU YA ARDHI
Mlonge una jumla ya virutubishi 92, mmea au mti mwingine wenye virutubishi vingi baada ya mlonge una virutubishi 28. Mlonge una viondoa sumu 46 na viondoa uvimbe mbalimbali mwilini 36, una asidi amino 18 na asidi amino mhimu zaidi 9 ambazo miili yetu haina uwezo wa kuzitengeneza.
Unga wa majani ya mlonge unao uwezo wa kutibu magonjwa zaidi ya 300 mwilini, magonjwa hayo ni pamoja na;
1. Huko Afrika magharibi madaktari hutumia mlonge kutibu Kisukari
2. Huko India mlonge hutumika kutibu shinikizo la juu la damu
3. Hutibu matatizo au maumivu ya mishipa
4. Hutuliza mapigo ya juu ya moyo (stroke),
5. Hutibu Kansa
6. Pumu
7. Hutuliza wasiwasi
8. Kikohozi
9. Maumivu ya kichwa
10. Inazuia na kushusha lehemu (cholesterol) hata ile ya juu zaidi (hypocholesteremia)
11. Inapunguza mafuta tumboni
12. Inaweka sawa homoni
13. Inatibu maumivu wakati wa hedhi (dysmenorrhea),
14. Unasafisha ini (hepatic detoxification),
15. Unasafisha mkojo na kibofu cha mkojo
16. Unarekebisha matatizo kwenye tezi
17. Unatibu kipindupindu na kuharisha
18. Kifua kikuu
19. Kichwa kizito
20. Uchovu
21. Mzio (aleji)
22. Vidonda vya tumbo
23. Maambukizi kwenye ngozi
24. Maumivu mbalimbali mwilini
25. Huondoa madoa doa meusi kwenye ngozi (blackheads),
26. Husafisha damu,
27. Hutibu matatizo kwenye koo
28. Huondoa makohozi mazito kooni
29. Huondoa taka na msongamano kifuani
30. Hutibu kipindupindu
31. Huondoa mtoto wa jicho au uvimbe kwenye jicho
32. Hutibu maambukizi kwenye macho na kwenye masikio
33. Unatibu homa
34. Maumivu kwenye maungio
35. Huondoa chunusi
36. Hutibu matatizo karibu yote ya ngozi na kinga ya mwili
37. Matatizo kwenye mfumo wa upumuwaji
38. Inatibu Kiseyeye (scurvy)
39. Huongeza uwingi wa mbegu za kiume na nguvu kwa ujumla
40. Unatibu minyoo
41. Huongeza maziwa kwa wingi kwa mama anayenyonyesha
42. Huondoa uvimbe kwenye utumbo mpana (colitis)
43. Unatibu gauti (dropsy),
44. Unatibu kuhara damu (dysentery)
45. Unatibu kisonono ( gonorrhoea)
46. Unatibu tatizo la kukosa usingizi,
47. Unatibu homa ya manjano (jaundice),
48. Unatibu malaria
49. Unatibu U.T.I na matatizo mengine kwenye mfumo wa mkojo
50. Unasidia pia kujenga na kuimarisha misuli
51. Unatibu magonjwa ya mifupa
Mlonge unasafisha mwili wako wote, unasafisha ini, figo, moyo, macho, unaimarisha meno, ngozi na nywele. Wakati unatumia mlonge unakufanya ujisikie vizuri, ujisikie mpya (fresh) na mwenye nguvu. Watu wengi wanaotumia mlonge huwa ni wenye afya nzuri hata kwa muonekano tu hata wanapokuwa na umri mkubwa zaidi ya miaka 90.
Majani ya mti wa mlonge pia yanaweza kutumika kutengeneza biogas (aina ya nishati ya umeme inayotokana na kinyesi cha ng’ombe au takataka). Hutumika pia kama chakula cha wanyama kama sungura, mbuzi, ng’ombe, mbwa nk. Sungura wanaonekana kupenda zaidi mlonge kuliko wanyama wote.

MBEGU ZA MLONGE
Image result for MBEGU ZA mlonge 
Image result for MBEGU ZA mlonge
MBEGU ZA MLONGE
1. Mbegu zake hutumika kama kiuaji sumu na pia hutibu uvimbe. Hutibu maumivu ya kwenye mishipa, baridi yabisi, gauti, kukamaa mishipa, magonjwa ya ngono na majipu. Mbegu hizi hukaangwa kidogo, hupondwapondwa na kuchanganywa na mafuta ya nazi na kupakwa sehemu yenye tatizo.
2. Mbegu za mlonge zilizokaangwa na mafuta yake husaidia watu wanaoshindwa kuzalisha mkojo.
3. Mbegu zake hutumika pia kumtuliza au kumfanya mtu mwenye kifafa a-‘relax’.
4. Mbegu za mti wa Mlonge ni kinga dhidi ya vijidudu (bacteria) wasababishao magonjwa na kuathiri ngozi ikiwemo fangasi.
5. Pia mbegu hutumika katika kusafisha au kuchuja maji ambapo zikipondwa na kuwekwa kwenye maji yenye tope au machafu husababisha uchafu kujikusanya na kuzama chini kisha kuacha maji yakiwa safi na salama kwa kupikia au kunywa badala ya kuchemsha.
6. Mbegu za mlonge pia huongeza kwa kiasi kingi kinga ya mwili (CD4), Kama una tatizo la kinga ya mwili wako kushuka basi tumia mbegu za mlonge kwa mwezi mmoja mpaka mitatu na kinga yako itaimarika sana.
Chukuwa punje 3 na uzimenye ganda lake la juu na utafune mbegu ile ya ndani yote hizo tatu na ukimaliza kuzitafuna kunywa maji ya kawaida siyo ya kwenye friji glasi 2 (nusu lita), fanya hivi kutwa mara tatu.
TUTAENDELEA KUKUJUZA ZAIDI KUHUSU FAIDA ZA MLONGE ENDELEA KUFUATILIA MAKALA ZETU KUPITIA HAPA THE BANTU
Share this post :

+ maoni + 5 maoni

26 Novemba 2020, 05:53

mbegu za mlongo hutibu mtu anaye ugua bawasiri ya ndani

27 Novemba 2020, 11:15

Nimefurahi sana namna ulivyoelezea kwa uufasaha mkubwa nilianza kusikia habari za mti huu wa mlonge ilikuwa miaka ya 2005 na nilipewa mbegu tatu na mzee mmoja nikatafuna kweli nilisikia na mwili wenye nguvu na tumbo likawa tulivu na hata sasa nimetafuna mbegu 3 najisijisi burudani ndani ya mwili wangu asante sana.

22 Januari 2021, 02:11

Bawasiri ya nje inatibiwa na majani au mzizi????

6 Machi 2021, 06:10

Nikitumia mbegu za mlonge nasikia kiungulia

8 Juni 2021, 04:18

MLONGE UNA MAMBO MBALIMBALI AMBAYO YANAFAIDA NYINGI NDANI YA MWILI WA MWANADAMU
*Kalsiamu mara 17 zaidi ya ile ya maziwa ya ng’ombe
*Potasiamu mara 15 zaidi ya ile ya kwenye ndizi
*Una vitamini A mara 10 zaidi ya ile ya kwenye karoti
*Una protini nyingi mara 9 zaidi ya ile ya kwenye mtindi (Yogurt)
*Una Klorofili (kemikali ya rangi ya kijani ipatikanayo katika mimea) mara 4 zaidi ya ile ya kwenye nyasi au majani ya ngano (wheatgrass)
*Una madini chuma (iron) mara 25 zaidi ya yale ya kwenye Spinach
*Una vitamini A mpaka Z,
*Una Omega 3, 6, na 9
*Una asidi amino zile mhimu zaidi zinazohitajika na mwili
*Una kiasi cha kutosha cha madini ya Zinc ambayo ni madini mhimu katika kuongeza homoni za kiume na nguvu za kiume kwa ujumla

Chapisha Maoni


Get This:Techkgp

PAGE VIEWERS

About Me

Blog Archive

Blog za rafiki zangu

Get This:Techkgp
3D Live Statistics
 
Support : The Bantu | Mufandish | Mufandish Inc
Copyright © 2011. MUFANDISH NEWS - All Rights Reserved
Template Created by Mufandish Inc Published by Mufandish Mufandish
Proudly powered by Blogger