Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Septemba, 2013

MAREKANI MKAMATENI RAIS BASHIRI (ICC)

Picha
Bashir ametishia kumfukuza balozi wa Marekani nchini Sudan Siku mbili baada ya Rais wa Sudan kuiomba Marekani kumpa Visa ya kusafiri nchini humo kuhudhuria mkutano wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York, wito umetolewa kwa taifa hilo kumkamata Bashir na kumkamabidhi kwa mahakama ya ICC. Mkutano huo utafanyika wiki ijayo. Ombi hilo limetolewa na ICC kwa Marekani na kuitaka impe Visa Bashir na kisha kumkamata na kumkabidhi kwa mahakama hiyo pindi tu atakapotua nchini humo. Bashir anatakikana na mahakama ya ICC kwa tuhuma za uhalifu dhidi ya binadamu na pia kuamuru mauaji ya halaiki katika jimbo la Darfur. Marekani ilisema kuwa ilipokea ombi la Bashir kutaka Visa na kulitaja ombi hilo kama la kuudhi na kejeli kubwa kwa taifa hilo. Ilimtaka Bashir kwanza kujikabidhi kwa mahakamya I...