- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Machapisho
Inaonyesha machapisho kuanzia Desemba, 2013
MAELFU YAMZIKA MHESHIMIWA MADIBA HUKO QUNU LEO
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Takriban watu 4,500 ikiwemo wageni wa kimataifa wanahudhuria mazishi hayo ambayo ni ya mchanganyiko wa tamaduni za kale na mambo ya kisasa. Familia ya Mandela ilikesha wakijiandaa kwa mazishi ya leo huku kukiwa na muimbaji ambaye atakuwa anaita mizimu ya mababu wa kale na pia wakiongelesha mwili wa Mandela kumwambia kuwa sasa anazikwa. Ni kuambatana na tamaduni na mila za watu wa ukoo wa Mandela wa Thembu. Viongozi wa Afrika, familia na marafiki wametoa heshima zao za mwisho kwa hayati Nelson Mandela katika mazishi yake ya kitaifa katika kijiji cha Qunu katika mkoa wa Cape Mashariki. Mandela alikuwa rais wa kwanza mzalendo wa Afrika Kusini. Rais Jacob Zuma amesema kuwa wakati safari ndefu ya Mandela kuelekea uhuru imekwisha, raia wa Afrika Kusini wana jukumu la kuendeleza sera zake na urithi wake. Takriban watu 4,500 ikiwemo wageni wa kimataifa wanahudhuria mazishi hayo ambayo ni ya mchanganyiko wa tamaduni za kale na mambo ya kisasa. Familia ya Mandela ilikesha wakijian...
MAELFU WAOMBOLEZA KIFO CHA MANDELA
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Nelson Mandela kuzikwa tarehe 15 Desemba Raia wa Afrika Kusini wako kwenye maombolezo kwa siku ya pili hii leo wakiwa kwenye mkesha kwa usiku nzima kwa ajili ya kuomboleza mpendwa wao Kiongozi wa zamani wa taifa hilo Nelson Mandela, aliyeaga dunia siku ya Alhamisi akiwa na umri wa miaka 95. Watu wamekuwa wakikumbuka mema yake , wakicheza na kuimba Mbele ya makazi yake ya zamani mjini Soweto. Katika mkutano na Waandishi wa habari , Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma aliainisha matukio ya juma zima kwa ajili ya maombolezo ambapo ametangaza kuwa siku ya jumapili siku maalum ya maombi na ibada maalum. Siku ya Jumanne, itakuwa ni siku ya shughuli maalum za maombolezo ya kitaifa ambapo shughuli hizo zitafanyika katika uwanja wenye uwezo wa kukusanya watu 95,000 ulio nje kidogo ya mji wa Jo...