Raia nchini Nigeria wakiandamana wakitaka wasichana waliotekwanyara kuwachiliwa huru.
Wakazi wa kaskazini mashariki mwa Nigeria wanasema
kuwa washukiwa na kundi la Boko haramu wamelilipua daraja moja karibu na
eneo ambalo wasichana 200 walitekwanyara yapata mwezi mmoja uliopita.
Daraja hilo lililopo katika barabara muhimu ni la pili kuharibiwa katika kipindi cha siku mbili.Inasemekana kuwa ulipuaji wa daraja hilo ni mpango wa wanamgambo hao kuwazuia wale wanaotaka kuwanusuru wasichana hao kutofika eneo hilo. Mke wa rais wa Marekani Michelle Obama ameelezea utekajinyara wa wasichana hao kama kitendo cha kihuni kinacholenga kudidimiza ndoto za wasichana hao.
Chapisha Maoni