CHAMA CHA ANC CHAIBUKA NA USHINDI MZITO

 
Rais wa Africa kusini Jacob Zuma akisherehekea ushindi wa chama cha ANC katika uchaguzi mkuu uliokamilika.

Tume ya uchaguzi nchini Afrika kusini imetangaza matokeo rasmi ya uchaguzi mkuu uliofanyika siku ya jumatano.

Imesema kuwa chama tawala cha ANC kilijipatia ushindi mkubwa wa asilimia 62.
katika hotuba yake kwa taifa Rais jacob Zuma amesema kuwa matokeo hayo ni ishara njema kwamba raia nchini humo wana imani na chama cha ANC na kwamba chama hicho kitatumia umaarufu wake kuimarisha maisha ya watu masikini nchini humo.
Amesema kuwa ushindi huo umeipa serikali yake uwezo wa kuimarisha ukuwaji wa uchumi pamoja na ubunifu wa ajira.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA ZA KIAFYA ZA KITUNGUU MAJI KATIKA MWILI WA MWANADAMU

UFAHAMU MMEA WA MLONGE NA NAMNA UNAVYOFANYA KAZI NDANI YA MWILI WA MWANADAMU