Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza, amegusia kuwa huenda akawania urais kwa muhula wa tatu licha ya upinzani kulalamika kuwa hatua kama hiyo itakuwa inakiuka katiba.
Bwana Nkurunziza alizungumza kuwa maelezo katika katiba kuhusu jambo hilo hayaeleweki kwa misingi hiyo na kwamba yanahitaji ufafanuzi. Alisema kuwa ikiwa chama chake kitamuomba kuwania urais kwa muhula wa tatu, litakuwa swala linalohitaji kufafanuliwa na mahakama ya kikatiba.
Hali ya wasiwasi ya kisiasa nchini Burundi katika miezi ya hivi karibuni kuhusu hatua ya serikali kujaribu kubadilisha katiba. Wanachama wa upinzani, baadhi ambao wamekamatwa, wanasema hatua hiyo itawakera wengi hasa kwa msingi ya kikabila.
Chapisha Maoni