MAJAMBAZI YAVAMIA KITUO KIDOGO CHA POLISI CHA KIMANZICHANA (MKURANGA) NA KUJERUHI MAASKARI POLISI WALIOKO KITUONI HAPO

Mwili wa askari baada ya kupigwa mapanga ya kichwa na majambazi hayo kabla ya kupelekwa hospitali

Na Azminah Khan:
Mnamo 11/06/14 majira ya 0100hrs huko kituo kidogo cha Kimanzichana Pwani, watu wasiojulikana waliojifanya kuwa ni raia wema waliingia kituo kidogo cha Polisi Kiman nanzi Chana huku wakikimbia wakiwa na silaha za jadi kiasi cha askari wa zamu kuamini kuwa ni watu wanaohitaji msaada. Cha kushangaza watu hao walimvamia askari mwenye silaha ambaye amefahamika kwa jina la JOSEPH NGONYANI na kuanza kumkatakata mapanga na hatimaye kupora silaha SMG ikiwa na risasi 30. Ndipo walipoanza kushambulia kwa risasi askari wengine na kufanikiwa kupora SMG ya pili na risasi 30. Hatimaye watu hao wakapora risasi za akiba 41 na kutoweka kusikojulikana. Askari Ngonyani alifariki dunia alipokuwa anapatiwa matibabu kwenye hospitali wilaya ya Mkuranga. Askari mwingine aitwaye VENANCE amejeruhiwa mgongoni kwa risasi ambayo bado imo ndani, na kwenye paja la mguu wa kulia. Mgambo Mariam alijeruhiwa kichwani, shingoni na kuvimba bega kutokana na kupigwa sana
mateke na kujeruhiwa mbavuni. Kwa mujibu wa mganga Mkuu wa zamu wa Hospitali hiyo aitwaye VERONICA MUSIME, anathibitisha askari huyo kufariki akiwa anapatiwa matibabu hapo Mkuranga wakati wengine wamekimbizwa Muhimbili kwa matibabu ya kina. Kazi ya Mungu haina makosa; vituoni tuwe makini sana na stahili hii ya ujambazi; HESHIMA PEKEE kwa marehemu na majeruhi hawa ni kuwapata watuhumiwa wote na silaha walizoiba bila kuchelewa. Bila kujali mkoa ulipo, taarifa za haraka tunatarajia kupata toka kwako kuhusiana na wahusika wa tukio hili. AMEN


Mwili wa Askari mara tu baada ya kujeruhiwa na mapanga na majambazi hayo

mwili huo kesho utasafirishwa na kupelekwa kijiji cha nyumbani kwa marehemu huko Songea

THE BANTU inawapa pole wafiwa wa marehemu askari huyu.
Share this post :

Chapisha Maoni


Get This:Techkgp

PAGE VIEWERS

About Me

Blog Archive

Blog za rafiki zangu

Get This:Techkgp
3D Live Statistics
 
Support : The Bantu | Mufandish | Mufandish Inc
Copyright © 2011. MUFANDISH NEWS - All Rights Reserved
Template Created by Mufandish Inc Published by Mufandish Mufandish
Proudly powered by Blogger