Hawa ni baadhi ya watu
waliohudhuria Mazishi ya marehemu Mzee Mushi hapo jana katika viwanja vya
Mwembe Yanga
Mzee Mushi alifanya mengi sana ambayo anastahiki kuigwa, kwani katika moja ya mambo aliyoyafanya ni kulea watoto yatima katika majumba yake mwenyewe binafsi, lakini pia kuwasomesha watoto hao kuanzia darasa la kwanza hadi vyuo vikuu na ametoa viwanja vingi kwa ajili ya ujenzi wa Madrasa na Misikiti pamoja na ofisi za kuendeshea maswala ya dini hapa nchini.
Mzee Mushi alifariki kutokana na maradhi yaliyokuwa ya kimsumbua kwa muda mrefu, na alifia Dubai akiwa safarini kuelekea India kwa ajili ya matibabu zaidi.
PICHA MBALIMBALI
Mwandishi wa THE BANTU akisalimiana na bingwa wa
uchumi nchini Mheshimiwa Profesa Ibrahim Lipumba mara tu baada ya kumaliza
kuswalia marehemu Mzee Mushi
Mwanadada Asia Iddi rafikiwa wa watoto wa marehemu
Mzee Mushi akiwa katika majonzi makubwa ya kuondokewa na Mzee wa rafiki zake
wapendwa
Hawa ni baadhi ya watu
waliohudhuria mazishi ya marehemu Mzee Mushi jana
Chapisha Maoni