
Muigizaji mkongwe wa hapa nchini Mzee Saidi Ngamba maarufu kama Mzee Small afariki dunia usiku wa leo katika hospitali ya taifa ya muhimbili ambapo alikuwa amelaza akifanyiwa matibabu hospitalini hapo.
Taarifa hizi zimethibitishwa na mtoto wa marehemu Ndugu Mahmoud Said amesema kuwa ni kweli Mzee Small amefariki jana majira ya saa nne (04) na nusu usiku hospitalini hapo ambapo alikuwa akifanyiwa matibabu
taratibu za mazishi zinaendelea kufanyika nyumbani kwake Tabata Dar Es Salaam, hivyo kadiri tutakapokuwa tunazipata taarifa kuhusu yanayoendelea katika msiba huu basi tatajulisha kupitia Blog yako hii ya THE BANTU.
Tunamuombea Mzee wetu huyu Allah aipokee roho yake na ailaze mahali pema peponi.

Chapisha Maoni