Marehemu Sheikh
Mohammed Idris ameuawa na watu wasiojulikana
Hali ya ulinzi
imeimarishwa mjini mombasa kufuatia kuuwawa kwa Muhubiri mmoja wa kiisilamu
mapema leo asubuhi.
Ripoti zinasema
muhubiri huyo ambaye ni mwenyekiti wa chama cha maimamu na wahubiri wa
kiislamu, Sheikh Mohammed Idris, aliuawa kwa kupigwa risasi na watu
wasiojulikana akiwa njiani kuelekea msikitini kwa sala ya asubuhi.
Kamishna mkuu wa jimbo
la pwani mwa Kenya Mombasa, Marwa amesema uchunguzi unaendelea ili kubainmisha
waliohusika na mauaji hayo na dhamira yao.
Kufikia sasa hakuna
mshukiwa yeyote aliyekamatwa kuhusiana na mauaji hayo. Mbarak hamisi ni
muadhini katika msikiti wa manyatta ana aelezea kilichotokea.
Muhubiri huyo amezikwa
leo alasiri chini ya ulinzi mkali wa polisi. Mauaji hayo ni mauaji ya hivi
karibuni zaidi ya kiongozi mwingine wa kidini.
Ripoti zinasema kuwa
muhubiri huyo alikuwa amepokea vitisho kutoka kwa vijana wenye itikadi kali za
kidini na tayari alikuwa ameelezea hofu juu ya maisha yake kwa vyombo vya dola.
'Alipinga itikadi kali za kidini'
Vijana wa Mombasa
wanasemekana kuanza kufuata itikadi kali za kidini zinazoenezwa na Al Shabaab
Sheikh Mohammed Idris,
alikisiwa kuwa miongoni mwa wahubiri wa kiislamu ambao wanapinga itikadi kali
za kidini. Wahubiri kadhaa
mashuhuri wenye itikadi kali nchini Kenya wameuawa katika hali ya kutatanisha
miaka ya hivi karibuni.
Baadi yao walituhumiwa
kuwachochea vijana kuwa na itakadi kali za kidini na pia kuwa na uhusiano wa
karibu na kundi la wanamgambo la al-Shabaab nchini Somalia. Hata hivyo wafuasi wa
wahubiri hao waliouawa wameielekezea lawana serikali kwa kuwalenga viongozi wao
na kutekeleza mauaji ya kidini kwa misingi ya kupambana na ugaidi.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametaja kifo chake kama pigo kubwa katika harakati
za serikali za kupambana na siasa za itikadi kali. Ubalozi wa Uingereza
mjini Nairobi pia umelaani mauaji hayo ni kutaja kama pigo kubwa katika haraka
za kupambana na ugaidi katika Pwani ya Kenya. Afisa mmoja wa cha
maimu ahmed Kassim amelaani mauaji hayo na kutaka serikali kuwahakikishia
usalama wakati wanapoendelea na majuku yao.
Kabla ya kifo chake
Sheikh Mohammed Idris, alikuwa ameitaka serikali kukabiliana na baadhi ya watu
wenye itikadi kali za kidini ndani ya msikiti hali ambayo ilisababisha baadhi
ya waumini kumuita msaliti. Alikuwa mwenyekiti wa
kamati ya msikiti mmoja maarufu ambao uongozi wake ulitwaliwa na vijana ambao
wanapinga mahubiri yake ya wastani.

Chapisha Maoni