Na Azmina Khan:
Moto mkubwa uliowaka usiku wa Jumatano huko Dar Es Salaam katika soko la karume umeteketeza mali zote ambazo zikiuzwa katika soko hilo, moto huo ambao hakikujulikana chanzo chake umeleta hasara kubwa sana kwa wafanya biashara wa soko hilo ambapo hakuna hata mfanya biashara mmoja ambae yeye ameweza kufanikiwa kuokoa mali yake, kwani moto ulikuwa ni mkali sana.
Moto huo ulikuwa tayari kufika katika kiwanda kilichopo jirani na soko hilo (BREWERIES) lakini kikosi cha zima moto kilofanikiwa kuzima moto ambao ulikuwa tayari kuelekea katika kiwanda hicho.
Chapisha Maoni