Alikamatwa na anakabiliwa na mashItaka kadhaa ikiwemo kosa la uhaini.
Mahakama moja nchini Pakistani
imemruhusu rais wa zamani
Pervez Musharraf kuondoka nchini humo.
Hata hivyo, Musharraf hataruhusiwa kuondoka mara moja nchini Pakistani kwa muda, kwani mahakama hiyo imeipa serikali siku 15 kubatilisha uamuzi huo katika mahakama kuu.
Musharraf alirudi Pakistan kutoka uhamishoni mwaka uliopita akiwa na nia ya kurudi katika ulingo wa siasa.
Alikamatwa na anakabiliwa na mashItaka kadhaa ikiwemo kosa la uhaini.
Chapisha Maoni