MAUAJI YA ALBINO NI AIBU KWA TANZANIA
Raisi wa Tanzania Jakaya Kikwete ameahidi kumaliza kabisa wimbi la mauaji ya Albino,na kusema kuwa waganga wa jadi wanahusishwa na mauaji hayo na kulitia aibu kubwa taifa lake lililoko Africa Mashariki. Wanaharakati wa haki za binaadamu wameeleza kuwa wimbi hilo limechukua uhai wa Albino sabini na tano nchini Tanzania tangu mwaka wa elfu mbili na viungo vyao kutumika katika masuala ya kishirikina. Raisi Jakaya Kikwete amesema kwamba hawezi kuruhusu hali hiyo iendelee kama ambavyo imekuwa ikitendeka kwa miaka iliyopita,haya ameyasema katika mazungumzo yake mapema wiki hii. Rais huyo anaamini katika ushirikiano kati ya serikali na wananchi, vita hii ya kuzuia mauaji ya watu wenye ualbino itafanikiwa kuepuka aibu hii kwa taifa la Tanzania. Inakadiriwa kuwa katika Tanzania nzima kuna Albino wapatao 200,000,na wengi wao hutambuliwa kutokana na rangi yao ya ngozi,macho na nywele zao . Waganga wa kienyeji huwaambia wateja wao kwamba viungo vya Albino huleta bahati ya kupendwa,mai...