Mkurugenzi Mtendaji wa Shule ya ST.
Emmanuel High School, Ernest Masaka, akizungumza katika mahafali ya saba
ya Kidato cha Nne yaliyofanyika Chamazi jijini Dar es Salaam jana.
Wengine kutoka kulia ni Mkuu wa shule hiyo, Khalid Simba, Diwani wa Kata ya Chamazi, Hemedi Karata ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye mahali hayo, Katibu wa Diwani huyo na Lucy Peter, mke wa Mkurugenzi wa shule hiyo.
Mkuu wa shule hiyo, Khalid Simba, akizungumza katika
mahafali hayo. Kutoka kulia ni Makamu Mkuu wa Shule, Ally Mkamba, Diwani wa Kata ya Chamazi, Hemedi Karata na Katibu wa Diwani
Taswira ya meza kuu kwenye mahafali hayo.
Wahitimu wa kidato cha nne wakionesha vyeti vyao.
Wahitimu hao wakionesha jinsi ya kujifunza somo la Sayansi hapo jana.
Walimu wa shule hiyo nao wakishiriki kwenye mahafali hayo hapo jana.
Katibu wa Diwani wa
Kata ya Chamazi, akimkabidhi cheti mhitimu, Winfrida Komba katika
mahafali hayo hapo jana. Kulia ni Mkuu wa shule hiyo, Khalid Simba.
Na Dotto Mwaibale
WAHITIMU wa Kidato cha Nne mwaka 2016
katika Shule ya St. Emmanuel iliyopo Chamazi jijini Dar es Salaam
wametakiwa kuzingatia elimu ili kutimiza ndoto za maisha yao badala ya
kujihusisha na vitendo viovu na utoro.
Mwito huo umetolewa na Diwani wa Kata ya
Chamazi, Hemedi Karata wakati akiwahutubia wanafunzi hao kwenye
mahafali ya saba ya kidato cha nne ya shule hiyo yaliyofanyika Dar es
Salaam jana.
"Zingatieni masomo yenu ili mtimize
ndoto za maisha yenu ya baadae, wazazi wenu wanawalipia ada ni vizuri
mkawaonesha mafanikio yenu katika elimu na sio tabia mbaya," alisema
Karata ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo.
Alisema kwa maisha ya leo bila ya kuwa
na elimu kuna changamoto kubwa ya maisha hivyo aliwaasa wahitimu hao
kufanya bidii ya kusoma hata watapokuwa kidato cha tano na sita na elimu
ya juu.
Mkurugenzi Mtendaji wa shule hiyo,
Ernest Masaka aliwaomba wazazi kushirikiana na uongozi wa shule katika
kuwalea wanafunzi hao wawapo nyumbani na shuleni.
"Ushirikiano baina ya wazazi, wanafunzi
na walimu ni muhimu sana katika kuwajengea wanafunzi mazingira mazuri ya
kupata elimu bora hivyo nawaombeni tuendelee kushirikiana," alisema
Masaka.
Mkuu wa shule hiyo, Khalid Simba alisema
shule hiyo imekuwa ikifanya vizuri kutokana na ushirikiano uliopo kati
ya wazazi, walimu na wanafunzi wenyewe.
Alisema licha ya shule hiyo kuwa na
mafanikio, changamoto ndogo ndogo zinakuwepo lakini wanajitahidi
kuzitatua kwa kushirikiana kwa pamoja na wazazi.
Ushauri na maoni ya Mwandishi.
Tujitahidi kuhakikisha tunasimamia na kuwalinda vijana wa shule ili waweze kufikia na kutimiza malengo yao.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
Chapisha Maoni