Parachichi ni tunda ambalo mti wake hujulikana kisayansi kama Persea amerikana.
Tunda hili lina aminika kuwa na asili kutoka jimbo la Puebla, bara
Amerika ya kusini kunako nchi ya Mexico. Ushahidi wa kale kabisa,
takribani miaka 10000 BC umeonyesha parachichi lilitumika katika jimbo
la Puebla nchini Mexico. Lakini kutokana na faida nyingi kiafya
zipatikanazo kwa ulaji wa tunda hili, tunda hili sasa hupatikana na
kutumika kwa lishe sehemu nyingi duniani hususani barani Afrika.
Parachichi ni tunda la pekee ukilinganisha na matunda mengine, kimsingi matunda mengine huwa yana wanga(carbohydrate) kwa wingi, wakati parachichi lina aina ya mafuta ambayo yana faida kwa afya.
Aina ya kirutubisho
|
Kirutubisho
|
Kiwango kilichopo
|
Vitamini
|
Vitamini A
|
7ug
|
Vitamini E
|
2.1ug
| |
Vitamini C
|
10mg
| |
Thiamine
|
0.1mg
| |
Niacini
|
1.7mg
| |
Vitamini B 6
|
0.3mg
| |
Folic acid
|
81ug
| |
Madini
|
Kalshamu
|
12mg
|
Phosphorasi
|
52mg
| |
Magnesiamu
|
29mg
| |
Potasiamu
|
599mg
| |
Munyu (Sodium)
|
7mg
| |
Chuma
|
0.6mg
| |
Zinki
|
0.6mg
| |
Shaba
|
0.2mg
| |
Manganizi
|
0.1mg
| |
Protini muhimu
|
TRP(Tryptophan)
|
25mg
|
THR(Threonine)
|
73mg
| |
ILE(Isoleucine)
|
84mg
| |
LEU(Leucine)
|
143mg
| |
LYS(Lysine)
|
132mg
| |
MET(Methionine)
|
30mg
| |
CYS(Cysteine)
|
27mg
| |
PHE(Phenylalanine)
|
232mg
| |
TYR(Tyrosine)
|
49mg
| |
VAL(Valine)
|
107mg
| |
ARG(Arginine)
|
88mg
| |
HIS(Histidine)
|
49mg
|
Parachichi katika tafiti nyingi limeonekana kuwa na faida katika afya ya
moyo. Wagonjwa wa moyo wamekuwa katika makatazo ya kutumia aina ya
mafuta ambayo yamekuwa yakichangia kuongezeka kwa lehemu katika
damu(mafuta hayo kitaalam kama polysaturated fat), na kuongeza matumizi ya mafuta yasiyoongeza lehemu katika damu (monosaturated fat).
Parachichi ni chanzo kizuri cha mafuta yasiyoongeza lehemu katika damu.
Utafiti unaonyesha kuwa matumizi ya mafuta haya katika parachi
hupunguza lehemu iliyo hatari ( kitaalam kama, Low density lipoprotein), na huchangia katika ongezeko la lehemu isiyo hatari( High density lipoprotein).
Madini ya Potasiamu ni aina ambayo huwa watu hawapati ya kutosha kutoka
katika vyakula. Parachichi lina kiwango kikubwa cha madini ya potassium
kuliko ndizi. Tafiti mbalimbali zimeonyesha kuwa matumizi ya madini haya
huambatana na kupungua kwa shinikizo la damu, shinikizo la juu la damu
laweza kupelekea mtu kupata kiharusi, shambulizi la moyo hata figo
kushindwa kufanya kazi.
Parachichi lina kiwango kikubwa cha fiba. Fiba ni kirutubisho kutoka
katika vyakula vya jamii ya mimea, fiba huwa hazimeng’enywi tumboni
lakini huwa zina umuhimu mkubwa sana, kama kusaidia kupunguza uzito wa
mwili, kusaidia urekebishaji wa kiwango cha sukari mwilini na kupunguza
hatari ya kupata magonjwa mengi mwilini. Kuna aina fulani ya fiba ambazo
huwa ni virutubisho kwa ajili ya bakteria wenye faida tumboni, hii
huimarisha kinga ya mwili na kusaidia mwili kufanya kazi katika kiwango
kinachotakiwa. Kwa kuwa parachichi lina kiwango kikubwa cha fiba,
husaidia kuboresha mmeng’enyo na kupata choo katika hali ya kawaida.
Aina ya mafuta na virutubisho tulivyoviona awali katika parachichi
vinasaidia afya ya ngozi yako. Husaidia ngozi yako kutokuwa kavu na kuwa
na unyevu unaotakiwa na kuifanya ngozi kuwa laini na yenye afya.
Vitamini C husaidia katika kusaidia uponaji haraka wa ngozi na kujijenga
upya kwa seli za ngozi zilizoharibika,husaidia kujenga elastini na collageniambazo ni muhimu katika ngozi. Uwepo wa virutubisho viondoavyo sumu(antioxidants)
katika parachichi kama carotenoidi na vitamini E, hutusaidia kutukinga
na mionzi mikali ya jua, kwa hiyo huzuia makunyanzi katika ngozi na
kuifanya ngozi yako kuwa na mwonekano mzuri wakati wote.
Tunda hili ni lishe bora kwa wale wenye kisukari. Parachichi lina
kiwango kidogo cha sukari ukilinganisha na matunda mengine. Pia uwepo wa
mafuta aina ya ‘monosaturated’ husaidia kuboresha ufanyaji kazi
wa homoni ya insulini, katika urekebishaji wa kiwango cha sukari
mwilini. Faida nyingine ni kuwa Vitamini C katika parachichi husaidia
kuimarisha mishipa ya damu na kuboresha kinga ya mwili ambayo ni faida
kubwa kwa wagonjwa wenye kisukari.
Faida katika afya ya uzazi ni dhahiri. Parachichi lina Vitamini E ambayo ni “antioxidant”
Potasiamu, Vitamini B6,Vitamini C ambazo hutusaidia kutukinga na
magonjwa ya moyo hata yale ya kisukari. Chochote kile kinachosaidia afya
ya moyo pia husaidia afya ya uzazi. Wanaume wenye magonjwa ya moyo na
kisukari huwa tatizo kubwa la upungufu wa nguvu za kiume.
Parachichi pia limeonekana kuwa na faida nyingi katika kuboresha afya ya
macho, viungo vya mwili na nyinginezo nyingi. Katika utafiti mmoja uko
Marekani, ulionyesha kuwa watu walao parachichi walionekana kuwa na afya
bora ukilinganisha na wale wasiokula parachichi. Waliokula parachichi
hawakupatwa na matatizo ya mmeng’enyo ukilinganisha na wale wasiokula. Matatizo ya mmeng’enyo huchangia watu kupatwa na magonjwa ya moyo na kisukari.
Unasubiri nini sasa? Anza kutumia matunda haya kuboresha afya yako.
Unapokwenda sokoni usisahau kununua parachichi.Faida ni nyingi
zitokanazo na ulaji wa tunda hili.
Chapisha Maoni