Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na mamia ya wanachama wa Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) kabla ya kufungua mkutano huo Mkuu wa (CWT )katika ukumbi wa Chimwaga mkoani Dodoma. Wanachama hao wa CWT walisimama na kushangilia mara baada ya ahadi ya Rais Dkt. Magufuli kuwaahidi kuendelea kutatua kero zao mbalimbali. Mamia ya Wajumbe wa Chama cha Walimu(CWT) wakishangilia ndani ya ukumbi wa Chimwaga wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akijibu kero zao mbalimbali walizoziwasilisha. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na baadhi ya wajumbe wa Chama cha Walimu CWT mara baada ya kuwahutubia katika ukumbi wa Chimwaga mjini Dodoma. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ameshikana mikono na viongozi wa muda wa CWT, Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako, Spika wa Bunge Job Ndugai, pamoja na ...