Machapisho

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AMSIMAMISHA KAZI MKURUGENZI WA MAMLAKA YA MAJI MKOANI LINDI

Picha
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akitoa maelekezo hapo jana WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Lindi (LUWASA), Mhandisi Adam Alexander (pichani mwenye mafaili) kwa kosa la matumizi mabaya ya ofisi pamoja na kushindwa kusimamia ujenzi wa kituo cha kuzalisha maji katika Manispaa ya Lindi. Waziri Mkuu amemkabidhi Mhandisi huyo kwa Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Lindi, Bw. Stephen Chami na kumuelekeza afanye uchunguzi zaidi juu ya suala hilo. Waziri Mkuu ametoa agizo hilo jana Jumatano, Oktoba 19, 2016  wakati alipotembelea mradi wa maji wa Ng'apa ambapo aliagiza nafasi hiyo ikaimiwe na Mkurugenzi Msaidizi wa mamlaka hiyo, Mhandisi Idrisa Sengulo. "Kamanda wa TAKUKURU fanya mapitio ya kina ya mshahara wake. Yeye anasema analipwa Wizarani, mimi najua analipwa na LUWASA. Angalia kazi aliyokwenda kuifanya Dar es Salaam kama inalingana na siku alizokaa,”  alisisitiza Waziri Mkuu. Mhandisi hiyo anakabiliwa na tuhuma mbalimbali...

FAIDA KUMI (10) ZITOKANAZO NA UNYWAJI WA TANGAWIZI

Picha
1.Huondoa Harufu mbaya ya kinywa. Tofauti na vyakula vingine kama kitunguu swaumu, tangawizi husaidia uwe na harufu nzuri pale unapopumua na kufanya maeneo yamdomo kuwa safi 2.Msukumo Wa Damu Tangawizi husaidia msukumo wa damu mwilini kwasababu huupa mwili joto ambalo mara nyingi mwili huhitaji wakati wa usukumwaji wa damu mwilini. 3.Huondoa Magonjwa ya Asubuhi Licha ya kuwa tiba ya magonjwa kama Kikohozi na Mafua, Tangawizi pia husaidia kupunguza magonjwa ya asubuhi kama uchovu, na mning’inio. Kwa akina mama wajawazito, Tangawizi huwapunguzia homa za asubuhi pindi wanapoamka, pia hutumika kama kichocheo cha utulivu. 4.Mfumo wa Chakula Husaidia mwili kunyonya virutubisho kwenye chakula. Hii husaidiana sana pale unapoamua kupunguza uzito wa mwili na kupata virutubisho vilivyo muhimu tu. 5.Kurekebisha Sukari ya Mwili Tangawizi husaidia katika kuweka sawa kiwango cha sukari kwenye damu. Wagonjwa wa Kisukari wanashauriwa kut...