MECHI YA KWANZA YA MUUMIZA KICHWA MOURINHO
Kocha wa Chelsea,Jose Mourinho amesema itakua vigumu kujizuia wakati atakapokaa rasmi katika benchi ya Stamford Bridge kwa pambano lao la kwanza la Ligi Kuu ya Premier dhidi ya Hull City. Mourinho aliyejunga tena na klabu hiyo kwa awamu ya pili mnamo mwezi wa Juni baada ya kuondoka mwaka September 2007. "Nitakapoingia katika uwanja wangu,kukaa katika benchi langu pamoja na watu wangu ,itabidi niwe mtulivu kidogo,"Alisema Mourinho,mwenye umri wa miaka 50. "Itanichukua dakika mbili tatu kutafakari na kabla ya kushughulikia pambano lenyewe ." Mourinho aliwasili mara ya kwanza Stamford Bridge mwaka 2004, wiki chache tu baada ya kuiongoza Porto ya Ureno kunyakua kombe la mabingwa wa Ulaya. Alishinda kombe kombe la FA na pia Ko...