Zaidi ya watu kumi na watano wameripotiwa kuuwawa
wakati maafisa wa usalama nchini Misri walipoanza operesheni ya
kuwatimua wafuasi wa rais aliyeng'olewa madarakani Mohammed Morsi,
waliokuwa wamekita kambi mjini Cairo.
Lakini vuguvugu la Undugu wa Kiislamu, Muslim
Brotherhood, ambalo linaunga mkono maandamano hayo limesema idadi ya
waliouwawa inazidi kumi na watano. Milipuko ya risasi ilisikika na magari ya kivita yametumika kuwatimua waandamanaji hao. Maafisa wa usalama walifyatua gesi ya kutoa machozi.
Maafisa wamesema kuwa kambi ya waandamanaji hao
katika Medani ya Nahda magharibi mwa mji wa Cairo imevunjwa na
waandamanaji kutawanywa. Wizara ya mambo ya ndani imesema kuwa operesheni
ya kusafisha barabara za mji huo inaendelea. Wanaharakati wanaomuunga
mkono bwana Morsi walifukuzwa hadi hifadhi ya wanyama pori iliyopo
karibu pamoja na chuo kikuu cha Cairo, kituo cha televisheni
kinachomilikiwa na serikali Nile TV kimesema.

Chapisha Maoni