SOMA MAKALA HII UONE JINSI SHIVJI ALIVYOPONDA MCHAKATO WA KATIBA MPYA
MWANASHERIA NGULI PROFESA ISSA SHIVJI Asema umehodhiwa na wanasiasa na kutahadharisha usipoangaliwa unaweza kuzaa machafuko. Dodoma. Mwanazuoni na Mwanasheria nguli, Profesa Issa Shivji ameuponda mchakato wa Katiba Mpya kuwa umehodhiwa na wanasiasa na kutahadharisha kuwa usipoangaliwa vizuri unaweza kusababisha machafuko. Aliyasema hayo jana mjini hapa alipokuwa akitoa mhadhara kwa Jumuiya ya Chuo Kikuu cha Dodoma, (Udom). Mhadhara huo uliandaliwa kama sehemu ya mafunzo kwa ajili ya wanafunzi wanaojiandaa kuhitimu masomo yao (Convocation ). Profesa Shiviji ambaye alitumia saa 1.15 kutoa mhadhara wake juu ya mchakato wa Katiba, alisema Bunge la Katiba lipo juu ya Bunge la Kawaida. Alisema katika historia ya Tanzania imewahi kuwa na mabunge mawili yaliyoandaliwa kupata Katiba, lakini yote hayakuwa na wabunge waliochaguliwa. “Tukiangalia katika historia hatukuwahi kuwa na Bunge la Katiba ambalo lilichaguliwa na wananchi. Safari hii tulikuwa ...