MRADI WA SHULE BORA NCHINI WAZINDULIWA MKOANI PWANI
WAZIRI wa Uingereza anayeshughulikia Afrika, Vicky Ford amesema ndoto yake Ni kuona ufadhili kutoka nchini humo unaleta matokeo chanya nchini Tanzania, kwa kuhakikisha Watoto wenye mahitaji maalum ,wenye Mazingira magumu na watoto wa kike wanapata elimu bora. Aidha amesema ufadhili huo kupitia Shirika la msaada la nchi hiyo, linalenga kufikia watoto milioni nne nchini. Akizindua mradi wa shule bora ,mkoa wa Pwani ukiwa Ni mwenyeji, Ford alisema jamii, Serikali, wadau wa elimu wanapaswa kushirikiana kurudisha wimbi la wanafunzi walioacha shule kwa changamoto mbalimbali waweze kuendelea na masomo. "Tutaweka kipaombele kwa watoto wenye mahitaji maalum,wanaoishi kwenye Mazingira magumu na watoto wa kike, kupata haki ya kuendelea kusoma katika Mazingira bora "alifafanua Ford. Awali Waziri wa elimu, prof.Adolf Mkenda Alieleza mradi huo umefadhiliwa na Uingereza kwa paundi milioni Tisa ,ambapo unafikia mikoa Tisa, ili kuhakikisha Watoto wote hata wenye changamoto mbalimbali wanapa...