MRADI WA SHULE BORA NCHINI WAZINDULIWA MKOANI PWANI

 WAZIRI wa Uingereza anayeshughulikia Afrika, Vicky Ford amesema ndoto yake Ni kuona ufadhili kutoka nchini humo unaleta matokeo chanya nchini Tanzania, kwa kuhakikisha Watoto wenye mahitaji maalum ,wenye Mazingira magumu na watoto wa kike wanapata elimu bora.


Aidha amesema ufadhili huo kupitia Shirika la msaada la nchi hiyo, linalenga kufikia watoto milioni nne nchini.

Akizindua mradi wa shule bora ,mkoa wa Pwani ukiwa Ni mwenyeji, Ford alisema jamii, Serikali, wadau wa elimu wanapaswa kushirikiana kurudisha wimbi la wanafunzi walioacha shule kwa changamoto mbalimbali waweze kuendelea na masomo.

"Tutaweka kipaombele kwa watoto wenye mahitaji maalum,wanaoishi kwenye Mazingira magumu na watoto wa kike, kupata haki ya kuendelea kusoma katika Mazingira bora "alifafanua Ford.

Awali Waziri wa elimu, prof.Adolf Mkenda Alieleza mradi huo umefadhiliwa na Uingereza kwa paundi milioni Tisa ,ambapo unafikia mikoa Tisa, ili kuhakikisha Watoto wote hata wenye changamoto mbalimbali wanapata fursa ya kusoma.

Alisema, mradi huu pia utaweza kuwaendeleza walimu kufundisha kwa ufanisi ili kuinua kiwango cha taaluma mashuleni.

"Mradi huu unaofadhiliwa na Uingereza unaendana na adhma ya Serikali kuboresha sekta ya elimu kwa kupitia mitaala ,sheria ya elimu ya mwaka 1978,kuangalia ubora wa walimu ,wakufunzi ,kuangalia miundombinu ikiwemo madarasa."alisisitiza Mkenda.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa TAMISEMI, David Silinde alishukuru kwa niaba ya Serikali ya awamu ya sita kwa ufadhili huo.

Silinde alisema kwamba, watahakikisha fedha za mradi zitasimamiwa kutekeleza kwa makusudio lengwa.

Mwanafunzi wa shule ya msingi Mkoani,darasa la sita Ramadhani Juma alibainisha Mradi utawanufaisha kuboresha elimu zaidi .


Share this post :

Chapisha Maoni


Get This:Techkgp

PAGE VIEWERS

About Me

Blog Archive

Blog za rafiki zangu

Get This:Techkgp
3D Live Statistics
 
Support : The Bantu | Mufandish | Mufandish Inc
Copyright © 2011. MUFANDISH NEWS - All Rights Reserved
Template Created by Mufandish Inc Published by Mufandish Mufandish
Proudly powered by Blogger