Machapisho

TAZAMA VICHWA VYA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI TAREHE 29 JULAI 2018

Picha

TAZAMA MABINGWA WA TANZANIA BARA WAKIJIFUA HUKO UTURUKI TAYARI KUELEKEA MSIMU MPYA WA LIGI 2018/19

NAIBU WAZIRI WA NISHATI BI SUBIRA MGALU AAGIZA WANAOWALIPISHA WANANCHI FOMU ZA KUOMBA KUVUTIWA UMEME KATIKA NYUMBA ZAO WARUDISHE PESA HIZO KWA WANANCHI HAO

Picha
Naibu waziri Bi Subira Mgalu mapema leo atoa agizo kwa viongozi wa Tanesco ambao wanawalipisha wananchi pesa za fomu ya maombi ya kuvutiwa umeme majmbani mwao leo alipotembelea wilayani Rufiji na kufanya uzinduzi wa mradi wa umeme wa REA awamu ya tatu mzunguko wa kwanza. Uzinduzi huo ulifanyika katika Shule ya Sekondari Kazamoyo iliyopo wilayani hapo katika kata ya Ikwiriri. Naibu waziri amesema kuwa hii ni sehemu ya ahadi za Mheshimiwa Rais kuwa atahakikisha umeme unaingia vijijini na ni kweli juhudi hizo zinaendelea kufanywa pamoja na kuwa wapo baadhi yao wanabeza jitihada hizi zinazofanywa na Mheshimiwa Rais katika kuhakikisha anayabadilisha maisha ya watanzania. Pia Meneja wa Tanesco Ikworiri ndugu Saidi nae ameeleza kuwa mradi huu unaendelea na sasa wamekamilisha katika kijiji cha kazamoyo na bado wanaendelea katika vijiji vya umwe kaskazini na hivi punde maeneo hayo yatakuwa ni yenyekukamilika.   Mheshimiwa Naibu Waziri akihutubia wakati wa uzinduzi wa REA awamu ya 3 ...

KOCHA ZANZIBAR HEROES AFUNGUKA KUHUSU MECHI YA NUSU FAINALI DHIDI YA UGANDA

Kuona video hii bofya hapa https://youtu.be/svSzRZYW3Jk

RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA MKUTANO MKUU WA CHAMA CHA WALIMU TANZANIA (CWT) MKOANI DODOMA

Picha
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na mamia ya wanachama wa Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) kabla ya kufungua mkutano huo  Mkuu wa (CWT )katika ukumbi wa Chimwaga mkoani Dodoma. Wanachama hao wa CWT walisimama na kushangilia  mara baada ya ahadi ya Rais Dkt. Magufuli kuwaahidi kuendelea kutatua kero zao mbalimbali.  Mamia ya Wajumbe wa Chama cha Walimu(CWT) wakishangilia ndani ya ukumbi wa Chimwaga wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akijibu kero zao mbalimbali walizoziwasilisha.   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na baadhi ya wajumbe wa Chama cha Walimu CWT mara baada ya kuwahutubia katika ukumbi wa Chimwaga mjini Dodoma.  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ameshikana mikono na viongozi wa muda wa  CWT, Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako, Spika wa Bunge Job Ndugai, pamoja na ...

MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA PILI 2016 HAYA HAPA

Picha
BOFYA HAPA KUONA MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA PILI 2016

TAZAMA MTU ALIYESHINDIKANA KUFANYIWA MATIBABU KWA SABABU YA UREFU

Picha
Ka Baraka Elias Mashauri mwenye umri wa miaka 35 mkazi wa Musoma mkoani Mara ameshindwa kupata matibabu katika Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) kutokana na urefu wake usio wa kawaida. Baraka anayesumbuliwa na tatizo ya nyonga ana kimo kirefu cha zaidi ya futi 7 na hii kufanya kushindwa kupatiwa matibabu kufuatia vifaa katika taasisi hiyo ikiwemo mashine za X- ray vitanda vya kufanyia upasuaji kuwa vifupi ukilinganisha na urefu wake. Tatizo hilo la nyonga linalomsumbua Baraka limemfanya ashindwe kutembea na kulazimika kutumia magongo ambayo anasema yanamtesa kutokana na urefu alionao. Akizingumzia jinsi watu wanavyomshangaa kutokana na urefu wake alisema kuwa kwake anaona fahari kwani ni maisha ambayo ameyazoea kila anapokwenda. Amesema kuwa hiyo haimpi shinda kwani anajua wanamshangaa kutokana na urefu wake kitu ambacho si kibaya. Kuhusu ugonjwa unaomsumbua na baada ya kushindikana kupatiwa matibabu nchini, Baraka ameomba wasamaria wema waweze kumsaida ili apatiwe mati...