Naibu waziri Bi Subira Mgalu mapema leo atoa agizo kwa viongozi wa Tanesco ambao wanawalipisha wananchi pesa za fomu ya maombi ya kuvutiwa umeme majmbani mwao leo alipotembelea wilayani Rufiji na kufanya uzinduzi wa mradi wa umeme wa REA awamu ya tatu mzunguko wa kwanza. Uzinduzi huo ulifanyika katika Shule ya Sekondari Kazamoyo iliyopo wilayani hapo katika kata ya Ikwiriri. Naibu waziri amesema kuwa hii ni sehemu ya ahadi za Mheshimiwa Rais kuwa atahakikisha umeme unaingia vijijini na ni kweli juhudi hizo zinaendelea kufanywa pamoja na kuwa wapo baadhi yao wanabeza jitihada hizi zinazofanywa na Mheshimiwa Rais katika kuhakikisha anayabadilisha maisha ya watanzania. Pia Meneja wa Tanesco Ikworiri ndugu Saidi nae ameeleza kuwa mradi huu unaendelea na sasa wamekamilisha katika kijiji cha kazamoyo na bado wanaendelea katika vijiji vya umwe kaskazini na hivi punde maeneo hayo yatakuwa ni yenyekukamilika.
Mheshimiwa Naibu Waziri akihutubia wakati wa uzinduzi wa REA awamu ya 3
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kazamoyo wakiwa makini kumsikiliza naibu waziri
Wananakijiji wakiwa makini kumsikiliza naibu waziri
Chapisha Maoni