Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Aprili, 2014

WAATHIRIKA WA SHAMBULIO LA MWAKA 1998 WALIPWA FIDIA TANZANIA

Picha
Hili ni shambulizi la kigaidi lililotikisa Tanzania mwaka 1998 Watanzania walioathirika na mlipuko wa mabomu katika ubalozi wa Marekani yaliyopangwa na Osama bin Laden mjini Dar es Salaam wameshinda kesi yao na sasa watalipwa fidia. Katika hukumu iliyotolewa na Jaji wa mahakama kuu ya Marekani Thomas Bates mjini Columbas, familia tisa za watu waliokufa na waliojeruhiwa watalipwa jumla ya dola laki nne na ishirini za Marekani. Hukumu hii inakuja kufuatia kesi iliyofunguliwa mwaka 2000 kwa msaada wa wanasheria wa kimarekani. Jaji aliyekuwa anasikiliza kesi hiyo, huyo alitoa hukumu ya awali tangu mwaka 2011 na kilichokuwa kimebaki ni utoaji wa fidia hiyo. Mmoja wa waathirika hao Judith Mwila ambaye mume wake alifariki katika mkasa huo, amesema kuwa yeye amepata taarifa hiyo kupitia kwenye gazeti tu. Msim...

BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI KUCHAFUKA

Picha
 Ni baada ya wabunge kumtaka kumuondoa spika wa bunge hilo madarakani Mgogoro wa uongozi umezuka katika Bunge la Afrika Mashariki ambapo wabunge wa bunge hilo wanakusudia kumwondoa madarakani spika wa bunge hilo. Tayari wabunge hao wameshakusanya saini 36 kutoka kwa wabunge 45 wa bunge hilo ambazo zinatakiwa kwa mujibu wa kanuni. Wabunge hao wanamlaumu Spika huyo kwa kukiuka kanuni za bunge pamoja kushindwa kuwashirikisha wabunge kwenye baadhi ya uamuzi. Akiongea na waandishi wa habari kiongozi wa wabunge hao kwa niaba ya wabunge wenzake wa bunge hilo Abudulla Ali Hassani Mwinyi, amesema wabunge hao wamefikia hatua hiyo ya kumwondoa spika huyo Margareth Zziwa kufuatia kukerwa na mwenendo wake. Tayari wabunge hao wameshapeleka hoja ya kumwondoa spika huyo kwa Katibu wa Bunge hilo ikiwa na sahihi za wabunge 36 ili kutimiza matakwa ya utaratibu unaotakiwa kwa mujibu wa kanuni za bunge hilo ili kuanzisha ...

SHAMBULIZI LA KUJITOA MUHANGA LAUA WATU 15 NIGERIA

Picha
Haya ndio maafa yaliyotokana na shambulizi la kujitoa muhanaga Nigeria Watu kumi na tano wameuawa na wengine kumi na saba kujeruhiwa katika shambulizi la kujitolea muhanga unaoshukiwa kutekelezwa na kundi la wapiganiji wa kislamu la Boko Haram Nigeria. Msemaji wa wizara ya ulinzi nchini humo amethibitisha shambulizi hilo lilifanyika nje ya mji wa Maiduguri katika jimbo la Borno. Msemaji wa wizara ya ulinzi bwana Chris Olukolade, amesema shambulio hilo lilitekelezwa na mtu aliyekuwa amebeba vilipuzi katika gari lake. Mlipuaji huyo wa kujitoa muhanga alijilipua na kusababisha vifo na uharibifu wa magari yaliyokuwa yameegeshwa pahala hapo. Watu wengine sita walojihusisha na shambulizi hilo waliuawa na vikosi vya usalama, na mmoja kutiwa mbaroni . Shirka la kutetea haki za kibinadamu la Amnesty International lilisema katika ripoti yake ya hivi punde kuwa watu wasiopungu...

RAIS JACOB ZUMA AJIELEZA KUHUSU NYUMBA YAKE

Picha
  Hii ndio nyumba ya Rais Jacob Zuma Nyumba hii iligharimu dola milioni 23 kwa ukarabati Rais Jacob Zuma anatarajiwa kufika mbele ya kamati ya Bunge la A-Kusini kujieleza kuhusu kashfa ya kufuja pesa za umma zilizotumiwa kukarabati nyumba yake ya kifahari. Ukarabati huo uligharimu dola million 23 na Bw Zuma ameamrishwa na mkaguzi au mlinzi wa mali ya umma nchini humo alipe baadhi ya pesa hizo. Zuma alisema Jumatatu kuwa sio sawa kwake kutakiwa alipe sehemu ya pesa zilizotumiwa kwa ukarabati wa nyumba yake kwani sio yeye aliayeamuru ukarabati huo. Alisema kuwa maafisa wa serikali ndio walioagiza ukarabati huo bila ya kumshauri. Zuma alizungumza kwa mara ya kwanza Jumatatu tangu kashfa hiyo kujulikana akisema kuwa halipi chochote kwani hakuomba afanyiwe ukarabati wa nyumba yake hiyo.

SHEIKH MAKABURI AUAWA MOMBASA KENYA

Picha
  Sheikh Aboubakar Shariff enzi ya uhai wake Sheikh Abubakar Shariff anayejulikana kwa jina lengine kama Makaburi, ameuawa. Duru zinasema kuwa Makaburi aliuawa katika mtaa wa Shanzu mjini Mombasa ambako alikuwa anaishi. Polisi wamekuwa wakimtuhumu Makaburi kwa kueneza itikadi kali za kiisilamu miongoni mwa vijana wa kiisilamu mjini Mombasa Pwani ya Kenya na kuchochea vitendo vya kigaidi. Pia amekuwa akituhumiwa kwa kusajili vijana kuenda kupigania kundi la wanamgambo la Al Shabaab nchini Somalia, madai ambayo Makaburi amekuwa akiyakanusha. Duru zinasema kuwa vijana wameanza kuzua vurugu katika msikiti wa Majengo, Mombasa kufuatia taarifa za mauaji ya mhubiri huyo mwenye utata. Taarifa za kifo cha Makaburi zilitolewa katika msikiti Musa ambao umekuwa kitovu cha vurugu kati ya maafisa wa usalama na vijana wanaodaiwa kuhubiri na kufuata ikitaka...