Sheikh Aboubakar Shariff enzi ya uhai wake
Sheikh Abubakar Shariff anayejulikana
kwa jina lengine kama Makaburi, ameuawa.
Duru zinasema kuwa Makaburi aliuawa katika mtaa wa Shanzu mjini Mombasa ambako alikuwa anaishi.
Polisi wamekuwa wakimtuhumu Makaburi
kwa kueneza itikadi kali za kiisilamu miongoni mwa vijana wa kiisilamu
mjini Mombasa Pwani ya Kenya na kuchochea vitendo vya kigaidi.
Pia amekuwa akituhumiwa kwa kusajili vijana
kuenda kupigania kundi la wanamgambo la Al Shabaab nchini Somalia, madai
ambayo Makaburi amekuwa akiyakanusha.
Duru zinasema kuwa vijana wameanza kuzua vurugu
katika msikiti wa Majengo, Mombasa kufuatia taarifa za mauaji ya mhubiri
huyo mwenye utata.
Taarifa za kifo cha Makaburi zilitolewa katika
msikiti Musa ambao umekuwa kitovu cha vurugu kati ya maafisa wa usalama
na vijana wanaodaiwa kuhubiri na kufuata ikitakadi kali za kiisilamu.
Haijulikani ni nani aliyemuua Makaburi
Chapisha Maoni