Hii ndio nyumba ya Rais Jacob Zuma
Nyumba hii iligharimu dola milioni 23 kwa ukarabati
Rais Jacob Zuma anatarajiwa
kufika mbele ya kamati ya Bunge la A-Kusini kujieleza kuhusu kashfa ya
kufuja pesa za umma zilizotumiwa kukarabati nyumba yake ya kifahari.
Zuma alisema Jumatatu kuwa sio sawa kwake kutakiwa alipe sehemu ya pesa zilizotumiwa kwa ukarabati wa nyumba yake kwani sio yeye aliayeamuru ukarabati huo.
Alisema kuwa maafisa wa serikali ndio walioagiza ukarabati huo bila ya kumshauri.
Zuma alizungumza kwa mara ya kwanza Jumatatu tangu kashfa hiyo kujulikana akisema kuwa halipi chochote kwani hakuomba afanyiwe ukarabati wa nyumba yake hiyo.
Chapisha Maoni