Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Septemba, 2016
Picha
Ptofesa Ibrahim Haruna Lipumba akizungumza na wafuasi wake BARAZA Kuu la Uongozi la Chama cha Wananchi (CUF), limetangaza kumfukuza uanachama Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba. Amefukuzwa kwa kile kilichoelezwa kuwa amekwenda kinyume na katiba ya chama na kufanya uasi kwa wanachama.  Akisoma uamuzi huo jana mbele ya waandishi wa habari katika ofisi ya chama hicho iliyopo Vuga mjini Zanzibar, Mjumbe wa Baraza hilo, Katani Ahmed Katani, alisema Baraza Kuu hilo limechukua uamuzi huo chini ya Kifungu cha Katiba Ibara ya 10 (1) (c) ambapo wajumbe wote wapatao 43 walipiga kura na kukubaliana na uamuzi huo. Katani alisema baraza hilo limemtia hatiani Profesa Lipumba kwa kitendo chake cha Septemba 24 mwaka huu, kuvamia ofisi ya chama akiwa na kikundi cha watu waliowaita wahuni na kuwapiga walinzi huku akisababisha uharibifu mkubwa wa mali za chama. Aidha alisema baraza hilo limesikitishwa na vitendo vya dharau vya Profesa Lipumba kwa ku...

PROFESA IBRAHIM HARUNA LIPUMBA AGOMEA MKUTANO WA BARAZA KUU LA UONGOZI CUF

Picha
Mgogoro  ndani ya Chama cha Wananchi (CUF) bado unafukuta ambapo jana Prof. Ibrahim Lipumba, aligomea mkutano wa Baraza Kuu la Uongozi la chama hicho ulioitishwa leo visiwani Zanzibar Alisema, taarifa zilizotolewa kwa vyombo vya habari kuhusu kufanyika kwa mkutano huo hazitambui kwa kuwa, mamlaka zinazohusika kuitisha kikao hicho hazijakidhi matakwa. Akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi Kuu ya chama hicho Buguruni jijini Dar es Salaam kupitia taarifa iliyoandaliwa na Magdalena Sakaya, Naibu Katibu Mkuu Bara aliyesimamishwa na chama hicho alisema, matakwa ya katiba hayakuzingatiwa. “Wajibu wa Kamati ya Utendaji ya Taifa utakuwa kuandaa.. agenda za Baraza Kuu la Uongozi la Taifa na kutayarisha na kuhifadhi mihtusari ya vikao vyote vya Mkutano Mkuu wa Taifa, Baraza Kuu la Uongozi la Taifa na vya kamati ya utendaji ya taifa yenyewe na kuwasilisha taarifa ya yatokanayo kutokana na utekelezaji wa maamuzi ya kikao kilichohusika kilichopita,” Prof. Lipumba am...

ZIARA YA WAZIRI MKUU MH. KASSIM MAJALIWA KATIKA WILAYA YA RUFIJI LEO JUMATATU SEPTEMBA 26 2016

Picha
ZIARA YA MH. WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA KATIKA WILAYA YA RUFIJI Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa ametembelea wilaya ya Rufiji leo Jumatatu Septemba 26 na kutoa agizo kwa Afisa Elimu wa Mkoa wa Pwani Bwana Yussuf Kipengele kupunguza walimu kutoka Kibaha na kuwaleta Rufiji kwa lengo la kufundisha masomo ya kidato cha tano na cha sita katika Shule za Mkongo na Utete. Mh. Majaliwa ametoa agizo hilo leo akiwahutubia wananchi wa wilayani hapo katika Jumba la Maendeleo baada ya kuibuliwa hoja hiyo na Mbunge wa Rufiji Mh. Mohammed Mchengerwa kwa kudai kuwa Wilaya ya Rufiji inakabiliwa na changamoto ya walimu pamoja na kuwa shule zipo ila walimu ndo hakuna. Waziri Mkuu ameagiza mpaka tarehe 4 Oktoba taarifa ya kupelekwa walimu Rufiji iwe imemfikia. Lakini pia baada ya kusema hayo Waziri Mkuu ametengua baadhi ya watumishi katika sekta ya Maliasili na Utalii na kuagiza kutovunwa tena kwa misitu mpaka vibali vipya vitakapofika. Mh. Waziri Mkuu pia aligusia swala la upungufu wa watum...