ZIARA YA WAZIRI MKUU MH. KASSIM MAJALIWA KATIKA WILAYA YA RUFIJI LEO JUMATATU SEPTEMBA 26 2016

ZIARA YA MH. WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA KATIKA WILAYA YA RUFIJI


Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa ametembelea wilaya ya Rufiji leo Jumatatu Septemba 26 na kutoa agizo kwa Afisa Elimu wa Mkoa wa Pwani Bwana Yussuf Kipengele kupunguza walimu kutoka Kibaha na kuwaleta Rufiji kwa lengo la kufundisha masomo ya kidato cha tano na cha sita katika Shule za Mkongo na Utete.

Mh. Majaliwa ametoa agizo hilo leo akiwahutubia wananchi wa wilayani hapo katika Jumba la Maendeleo baada ya kuibuliwa hoja hiyo na Mbunge wa Rufiji Mh. Mohammed Mchengerwa kwa kudai kuwa Wilaya ya Rufiji inakabiliwa na changamoto ya walimu pamoja na kuwa shule zipo ila walimu ndo hakuna. Waziri Mkuu ameagiza mpaka tarehe 4 Oktoba taarifa ya kupelekwa walimu Rufiji iwe imemfikia.

Lakini pia baada ya kusema hayo Waziri Mkuu ametengua baadhi ya watumishi katika sekta ya Maliasili na Utalii na kuagiza kutovunwa tena kwa misitu mpaka vibali vipya vitakapofika.

Mh. Waziri Mkuu pia aligusia swala la upungufu wa watumishi katika sekta mbalimbali za utumishi wa uma, amesema kuwa mara baada ya kumalizika kwa zoezi la uhakiki wa watumishi hewa serikali itaangali mapengo katika baadhi ya sekta na mara kutangaza ajira.

Kuhusu swala la barabara iunganishayo Nyamwage hadi Utete kujengwa kwa kiwango cha lami, Mh Majaliwa amesema bajeti yake isubiriwe mwakani kwani kwenye bajeti hii halikuwekwa hivyo itakuwa ngumu sana kushughulikiwa kwa kipindi hiki.

Lakini pia kuhusu swala la umeme, imeonekana kuwa Rufiji kuna tatizo kubwa la kukatika kwa umeme mara kwa mara, hivyo basi Mh Majaliwa amesema kuwa hilo swala la kukatika kwa umeme analifahamu na kusema kuwa hivi punde tu litakaa sawa kwani kuna mtambo mmoja umesumbua ndo mana umeme unakatika mara kwa mara ila tayari wameshafanya utaratibu wa kuleta mtambo mpya na kuanza kutoa huduma ya umeme pasipo  an kukatika katika.

Kuhusu swala la migogoro ya wakulima na wafugaji Mh. Majaliwa amempa meno mkuu wa wilaya hiyo kuhakikisha anawachukulia hatua wenyeviti wa kijiji na watendaji ambao hawawajibiki ipasavyo katika ushughulikiaji wa migogoro hiyo. Hivyo basi wenyeviti na watendaji wa vijiji wameagizwa kulisimamia hili na endapo hawatawajibika basi mkuu wa wilaya awashughulikie ipasavyo.






Waziri Mkuu Mh Kassim Majaliwa akisalimiana na Mzee Ngwele wakati alipokuwa katika viwa vya FDC Rufiji



 Mh. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Halmashauri ya Wila ya Rufiji leo mara baada ya kuwasili wilayani hapo.

Mh. Kassim Majaliwa akipokea magodoro kumi (10) kutoka kwa mkuu wa chuo cha maendeleo ya jamii Ikiwirri Rufiji Bi. Cecilia Mfuko ikiwa ni sehemu ya kuchangia katika kituo cha afya kilichopo wilayani hapo.
Share this post :

Chapisha Maoni


Get This:Techkgp

PAGE VIEWERS

About Me

Blog Archive

Blog za rafiki zangu

Get This:Techkgp
3D Live Statistics
 
Support : The Bantu | Mufandish | Mufandish Inc
Copyright © 2011. MUFANDISH NEWS - All Rights Reserved
Template Created by Mufandish Inc Published by Mufandish Mufandish
Proudly powered by Blogger