Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Novemba, 2016

TAZAMA MTU ALIYESHINDIKANA KUFANYIWA MATIBABU KWA SABABU YA UREFU

Picha
Ka Baraka Elias Mashauri mwenye umri wa miaka 35 mkazi wa Musoma mkoani Mara ameshindwa kupata matibabu katika Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) kutokana na urefu wake usio wa kawaida. Baraka anayesumbuliwa na tatizo ya nyonga ana kimo kirefu cha zaidi ya futi 7 na hii kufanya kushindwa kupatiwa matibabu kufuatia vifaa katika taasisi hiyo ikiwemo mashine za X- ray vitanda vya kufanyia upasuaji kuwa vifupi ukilinganisha na urefu wake. Tatizo hilo la nyonga linalomsumbua Baraka limemfanya ashindwe kutembea na kulazimika kutumia magongo ambayo anasema yanamtesa kutokana na urefu alionao. Akizingumzia jinsi watu wanavyomshangaa kutokana na urefu wake alisema kuwa kwake anaona fahari kwani ni maisha ambayo ameyazoea kila anapokwenda. Amesema kuwa hiyo haimpi shinda kwani anajua wanamshangaa kutokana na urefu wake kitu ambacho si kibaya. Kuhusu ugonjwa unaomsumbua na baada ya kushindikana kupatiwa matibabu nchini, Baraka ameomba wasamaria wema waweze kumsaida ili apatiwe mati...

BREAKING NEWS: ALIYEKUWA WAZIRI WA ELIMU WA ZAMANI NA MBUNGE WA MUFINDI MH. JOSEPH MUNGAI AFARIKI DUNIA JIONI YA LEO

Picha
Habari zilizotufikia hivi punde kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, zinasema kuwa Aliyewahi kuwa Waziri wa elimu na Utamaduni katika Serikali ya Benjamin W. Mkapa ndugu Joseph Mungai, amefariki dunia majira ya saa 11 jioni.   Akithibitisha taarifa hizo, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Aminiel Aligaesha, alisema kuwa marehemu Mungai alifikishwa Hospitalini hapo leo baada ya kula kitu kibaya kinachodhaniwa 'Sumu' na kutapika mfululizo hali iliyompelekea kupoteza maisha.    Mwili wa marehemu umehifadhiwa Chumba cha maiti katika Hospitali hiyo ya Taifa ya Muhimbili. Habari kamili ya msiba huo zitawajia kadri zitakavyokuwa zikitufikia.

IFAHAMU HISTORIA YA MAREHEMU SAMWEL SITTA KWA UFUPI

Picha
Samuel John Sitta alizaliwa Desemba 18, 1942 huko wilayani Urambo Mkoa wa Tabora. Sitta alisoma Shule ya Msingi Urambo kati ya mwaka 1950 – 1953, kisha alikwenda Wilaya ya Sikonge mwaka 1954 - 1957 na kuendelea na masomo ya “Middle School” katika shule ya “Sikonge Middle School”. Baadaye mwaka 1958 – 1963 alianza masomo ya sekondari Shule ya Wavulana Tabora yaani “Tabora Boys” kidato cha I – IV na cha V – VI. Mara tu baada ya kuhitimu masomo ya sekondari, Sitta alijiunga Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kusomea Shahada ya Sheria (L LB) mwaka 1964 na kuhitimu mwaka 1971. Sitta amesoma shahada yake kwa miaka 7 kwa sababu mwaka 1966, wakati yuko mwaka wa pili na akiwa kiongozi wa wanafunzi UDSM, wanafunzi waligoma na kuandamana kupinga kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na kukatwa mishahara yao baada ya JKT. Hoja ya wanafunzi ilikuwa na mantiki kubwa, kwamba mbona vigogo wa serikali na wanasiasa wanalipwa mishahara minono na marupurupu makubwa? Baada ya shin...

TANZIA: ALIYEKUWA SPIKA WA BUNGE LA TANZANIA MH. SAMWEL SITTA AFARIKI DUNIA USIKU WA KUAMKIA LEO

Picha
 Mheshimiwa Samwel Sitta akiwa katika moja ya vikao Vya binge akizungumza enzi ya uhai wake Mheshimiwa Samwel Sitta afariki dunia huko nchini Ujerumani alipokwenda kwa ajili ya kufanyiwa matibabu. Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli ametuma salami za Rambirambi bungeni.  Rest In Peace Mh. Samwel Sitta. Kuwa nasi muda wote ili tuwe tunakueleza kila linalojiri

(MUENDELEZO) HUTAZEEKA MAPEMA ENDAPO UTATUMIA MMEA WA MLONGE

Picha
MAAJABU YA MMEA WA MLONGE Matatizo mengi ya kiafya ni matokeo ya lishe yenye viinilishe duni au hafifu jambo linalopelekea kuwa na kinga ya mwili isiyo na nguvu kupigana na magonjwa mbalimbali. Unaporekebisha usawa huo usio sawa wa kinga yako ya mwili kwa kutumia mimea na lishe zingine mhimu za asili hutakawia kuona matokeo mazuri kwenye afya yako. Uwezo wa mti wa mlonge kuyaweza yote hayo ni kutokana na kuwa na vitamini, madini mbalimbali na viondowaji sumu vingi kuliko mmea mwingine wowote. Wagonjwa wengi wenye UKIMWI katika sehemu nyingi za afrika magharibi wameripoti kuongezeka kiasi kikubwa cha kinga yao ya mwili baada ya kutumia mlonge kiasi cha kutokuhitaji dawa. NGUVU, UMAKINI, NGOZI YENYE KUPENDEZA, KUTOZEEKA MAPEMA NA KUPUNGUZA UZITO NA UNENE Mlonge una viinilishe mhimu vinavyosaidia kuuongezea uwezo mfumo wa mmeng’enyo wa chakula. Vitamini, madini na homoni mhimu zilizomo kwenye mti huu huufanya mwili wako kuwa na usawa unaohitajika kiafya na hivyo kukupa...

TAZAMA MAHOJIANO YA MH. RAIS MAGUFULI NA WAANDISHI WA HABARI ULIOFANYIKA IKULU DAR ES SALAAM LEO

Picha
BOFYA HAPA KUONA KWA PICHA AU ENDELEA KUONA KATIKA MAANDISHI     Rais Magufuli: Niwashukuru sana kwa michango yenu mikubwa katika maeneo yenu ya kazi. Swali(Tido Mhando): Ulichukua muda kuunda baraza la mawaziri, Je Katika tathmini hiyo wanafanya kazi kulingana na ulichotegemea wakifanye Jibu(Magufuli): Serikali niliyounda imenisaidia sana na wanafanya kazi zao vizuri, niliona niwe na baraza la watu wachache katika kuwatumikia wananchi, changamoto zipo lakini nina imani kubwa. Swali(Lulu Sanga TV 1): Kuna changamoto kubwa sana ya dawa, watoto wengi wanakufa kutokana na kukosa dawa, unaoneje ukibana matumizi kupata dawa ukazigawa hospitali kubwa au kampeni kama ile ya madawati. Jibu(Rais Magufuli): Katika bajeti yetu tumetenga bilioni 1.99 na tumeongeza bajeti ya kununulia madawa karibu mara kumi. Tumebadilisha utaratibu badala ya kununua kutoka kwa suppliers sasa tunanunua moja kwa moja kutoka viwandani pia kuna nchi zinataka kuwekez...