MAAJABU YA MMEA WA MLONGE
Matatizo mengi ya kiafya ni matokeo ya lishe
yenye viinilishe duni au hafifu jambo linalopelekea kuwa na kinga ya mwili
isiyo na nguvu kupigana na magonjwa mbalimbali. Unaporekebisha usawa huo usio
sawa wa kinga yako ya mwili kwa kutumia mimea na lishe zingine mhimu za asili
hutakawia kuona matokeo mazuri kwenye afya yako.
Uwezo wa mti wa mlonge kuyaweza yote hayo ni
kutokana na kuwa na vitamini, madini mbalimbali na viondowaji sumu vingi kuliko
mmea mwingine wowote. Wagonjwa wengi wenye UKIMWI katika sehemu nyingi za
afrika magharibi wameripoti kuongezeka kiasi kikubwa cha kinga yao ya mwili
baada ya kutumia mlonge kiasi cha kutokuhitaji dawa.
NGUVU, UMAKINI, NGOZI YENYE KUPENDEZA,
KUTOZEEKA MAPEMA NA KUPUNGUZA UZITO NA UNENE
Mlonge una viinilishe mhimu vinavyosaidia
kuuongezea uwezo mfumo wa mmeng’enyo wa chakula. Vitamini, madini na homoni mhimu
zilizomo kwenye mti huu huufanya mwili wako kuwa na usawa unaohitajika kiafya
na hivyo kukupa kinga dhidi ya magonjwa mengi bila idadi.
Mlonge una kiinilishe mhimu sana kwa wingi kuliko
mmea au mti mwingine wowote duniani mara maelfu kadhaa kiitwacho kwa kitaalamu
kama ‘Zeatin’. Zeatin ndiyo hutengeneza seli mpya za ngozi pia huzifanya seli
mpya kutengenezwa kwa haraka na kwa wingi zaidi ya zile seli zinazokufa. Hii
huleta matokeo mazuri ikiwemo kuondoa mikunjo ya ngozi au ngozi kuzeeka sehemu
za uso na sehemu nyingine za mwili na kukupa afya nzuri ya ngozi.
Kwenye mlonge kuna ‘Sulfur’, hii sulfur ni mhimu
katika kuunda vitu mhimu kwenye ngozi kama collagen na keratin huku viuaji au
viondowaji sumu zaidi ya 30 vinavyopatikana kwenye mlonge ni mhimu kwa ajili ya
afya ya ngozi yako.
Mlonge ambao umekuwa ukitumika kwenye vituo vingi
vinavyojihusisha na kupunguza uzito huwa una nguvu ya
asili ya kupunguza njaa, huuongezea nguvu mfumo wa mmeng’enyo wa chakula na
kukung’arisha wewe huku ukikuacha na virutubishi vingi mhimu zaidi.
HUIRUDISHA UPYA AFYA YA MWILI WAKO;
Baada ya kufikisha umri wa miaka 30 hivi nguvu
zako za mwili huanza kushuka. Mwili wako utaanza kuleta mchonyoto. Utaona
unaanza kupoteza umakini nyakati za mchana sababu hukuzingatia nini ule wakati
ulipokuwa kijana. Baadhi ya kuharibika kwa afya hakuwezi kurudishwa nyuma ikiwa
ni pamoja na kuzorota kwa afya ya meno.
AFYA MBOVU YA MENO INAPELEKEA MAGONJWA KADHAA
NA VIFO;
Calcium, Magnesium, Manganese, Potassium, Boron
na Vitamini D yote ni madini mhimu ili uwe na meno yenye afya. Magonjwa mengi
sugu ni matokeo ya upasuaji wa kwenye kinywa. Kila mtu anapaswa kulinda afya ya
meno yake kuanzia leo kwani meno yakishaoza au kuharibika huwa ni vigumu kupona
na kurudi kwenye hali yake ya mwanzo. Afya ya meno yako itaamua ni miaka
mingapi unaweza kuishi.
Kila mmoja wetu anatakiwa kutimiza wajibu wake
linapokuja suala la afya ya mwili wako. Tumia google tafuta taarifa za kile
unachokula au kunywa kila siku. Kichwa kitakuuma utakapojua ni nini unakula!.
Nenda YouTube angalia video hizi: “Food Matters” na “Dying to have know”.
Tafuta kwenye chaneli ya Discovery movie inaitwa “Moringa The Miracle Tree” na
video nyingine inaitwa ‘Moringa Oleifera’.
BIDHAA NYINGI ZA AFYA HAZINA AFYA YOYOTE;
Bidhaa nyingi za afya hazina utafiti halisi
(genuine) unaojitegemea au zina maelezo kutoka kwa mtengenezaji tu wa hiyo
bidhaa. Mlonge una mfululizo wa tafiti za watu wengi na shuhuda za watu kote
duniani zaidi ya miaka 4000 iliyopita. Ni mtishamba kwa asilimia 100 unaoota
wenyewe.
Matumizi ya mlonge kama kiua vijasumu
(antibiotic) kwenye tiba asili yalianza miaka maelefu iliyopita. Mlonge
ulitumika kwa mara ya kwanza kama dawa zaidi ya miaka 2000 kabla ya Kristo.
Watabibu wazamani wa Misri na Ugiriki waliona faida nyingi za mti huu na
wakautambulisha kwa Warumi na baadaye mlonge ukaenea mashariki mwa India na
sehemu ya chini ya nchi ya Uchina, kusini mashariki mwa Asia na Ufilipino na
magharibi mwa Misri kuzunguka mediterania na mwishowe ukafika kwa Wahindi
mashariki mwa Amerika. Leo zaidi ya watu milioni 400 wanatumia mlonge. Shirika
la afya duniani (W.H.O) limekuwa likitumia mlonge zaidi ya miaka 40 sasa.
Unga wa majani ya mlonge unapaswa uwe ni wa
kijani kweli kweli na majani yake yawe yalianikwa kivulini na siyo juani. Anza
na kijiko kidogo kimoja ukichanganya na vimiminika kama maji ya uvuguvugu au
juisi yoyote ya matunda uliyotengeneza mwenyewe nyumbani kutwa mara moja na
taratibu ongeza kiasi cha dawa kadri unavyohitaji. Unaweza kuuchanganya pia
kwenye wali wakati unakula au unaweza kuweka ndani ya kikombe cha uji au
unaweza kutumia kama majani yako ya chai ingawa hautakiwi uchemshe sana kwenye
moto.
Mti wa mlonge sasa umeanza kuwa maarufu huko
Marekani hii ni kutokana na mti wenyewe kuendelea kupata umaarufu miongoni mwa
watu wanaojali afya zao. Ingia google andika ‘Moringa plants for sale’
utagundua keyword hiyo inatafutwa kila siku mara maelfu. Watu wengi pia
wameanza kilimo cha mlonge kama biashara ya kuwaingizia kipato. Ukiwa na miti
200 tu ya mlonge shambani kwako tayari wewe siyo mwenzetu.
Mti wa mlonge ni moja ya miti mhimu katika sehemu
yote ya dunia. Kadri watu wanavyoendelea kuutafiti na kuusoma mti huu ndivyo
mahitaji ya unga wa majani yake, mbegu zake, unga wa mbegu zake na mafuta ya
mbegu zake yatakavyozidi kuongezeka na kuongezeka
Chapisha Maoni