BREAKING NEWS: ALIYEKUWA WAZIRI WA ELIMU WA ZAMANI NA MBUNGE WA MUFINDI MH. JOSEPH MUNGAI AFARIKI DUNIA JIONI YA LEO
Habari
zilizotufikia hivi punde kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili,
zinasema kuwa Aliyewahi kuwa Waziri wa elimu na Utamaduni katika
Serikali ya Benjamin W. Mkapa ndugu Joseph Mungai, amefariki dunia
majira ya saa 11 jioni.
Akithibitisha taarifa hizo, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma
katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Aminiel Aligaesha, alisema
kuwa marehemu Mungai alifikishwa Hospitalini hapo leo baada ya kula kitu
kibaya kinachodhaniwa 'Sumu' na kutapika mfululizo hali iliyompelekea
kupoteza maisha.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa Chumba cha maiti katika Hospitali hiyo ya Taifa ya Muhimbili.
Habari kamili ya msiba huo zitawajia kadri zitakavyokuwa zikitufikia.
Maoni
Chapisha Maoni