Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Aprili, 2023

CHAMA CHA SKAUTI TANZANIA WILAYA YA RUFIJI KATIKA KUADHIMISHA SIKUKUU YA MUUNGANO WAMETEMBELEA KITUO CHA AFYA KUWAFARIJI WAGONJWA

Picha
Na: Yussuf Yussuf Chama cha Skauti Wilaya ya Rufiji mapema leo hii wametembelea kituo cha afya cha Ikwiriri kwa lengo la kuwatembelea wagonjwa na kuwafariji ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya sherehe za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Chama hicho ni dasturi yao kwa kila matukio ya kitaifa yanapotokea hufanya mambo kama haya ya kujitolea kama ilivyo utamaduni wao. Sambamba na hilo wameweza kupata kujifunza historia hii ya Muungano kutoka kwa wazee walioushuhudia Muungano huo .  

MBUNGE WA JIMBO LA RUFIJI AFUTURISHA MAELFU YA WANANCHI IKWIRIRI RUFIJI

Picha
IKWIRIRI RUFIJI-PWANI  SIKU YA JANA MAWAIDHA YA MBUNGE WA RUFIJI KABLA YA MUDA WA IFTARI. Mbunge wa Rufiji na Waziri wa Mali Asili na Utalii Nchini  Mhe, Mohamed Mchengerwa Kupitia Wana Rufiji Atoa Shukrani za dhati kwa Mhe, Rais Samia Suluhu kuendelee kumtakia kheri kuwa na Afya Njema na Upendo wa dhati kwa Wana Rufiji na Watanzania wote  katika  Kutekeleza Majukumu yake na Maendeleo anayoendelea kuwaletea Wana Rufiji Ameyasema hayo mbele ya wananchi wa Tarafa ya ikwiriri. Ikiwa ni siku ya Pili ya Kufuturisha Wananchi na Wakazi wa Rufiji, Siku ya  Jana Wamejitokeza  wananchi takriban 8500 kwenye Futari ya Ikwiriri ikitanguliwa na Futari ya Utete ya Tarehe 8/4. Aidha Mhe Mchengerwa amewasisitiza wana Rufiji pamoja na Mfungo Mtukufu wa Ramadhani kuzingatia Ibada muhimu ya kufanya Kazi kwani kwa mujibu wa mafundisho ya Dini ya Kiislamu , Kazi ni Ibada iliyotiliwa mkazo na Allah sw na mtume wake Mohammed  saw, hivyo shime kwa wana Rufiji kufanya kazi kwa ...