MBUNGE WA JIMBO LA RUFIJI AFUTURISHA MAELFU YA WANANCHI IKWIRIRI RUFIJI


IKWIRIRI RUFIJI-PWANI 

SIKU YA JANA MAWAIDHA YA MBUNGE WA RUFIJI KABLA YA MUDA WA IFTARI.

Mbunge wa Rufiji na Waziri wa Mali Asili na Utalii Nchini  Mhe, Mohamed Mchengerwa Kupitia Wana Rufiji Atoa Shukrani za dhati kwa Mhe, Rais Samia Suluhu kuendelee kumtakia kheri kuwa na Afya Njema na Upendo wa dhati kwa Wana Rufiji na Watanzania wote  katika  Kutekeleza Majukumu yake na Maendeleo anayoendelea kuwaletea Wana Rufiji Ameyasema hayo mbele ya wananchi wa Tarafa ya ikwiriri. Ikiwa ni siku ya Pili ya Kufuturisha Wananchi na Wakazi wa Rufiji, Siku ya  Jana Wamejitokeza  wananchi takriban 8500 kwenye Futari ya Ikwiriri ikitanguliwa na Futari ya Utete ya Tarehe 8/4.

Aidha Mhe Mchengerwa amewasisitiza wana Rufiji pamoja na Mfungo Mtukufu wa Ramadhani kuzingatia Ibada muhimu ya kufanya Kazi kwani kwa mujibu wa mafundisho ya Dini ya Kiislamu , Kazi ni Ibada iliyotiliwa mkazo na Allah sw na mtume wake Mohammed  saw, hivyo shime kwa wana Rufiji kufanya kazi kwa bidii na kuwaahidi yakuwa milango ya kumfikia yeye iko wazi na lengo kuu ni kubadili kabisa hali za kiuchumi na kuboresha maisha ya wana Rufiji .

Mwisho Mhe Mchengerwa Amewaomba  wana Rufiji Waendelee kupendana, kushikamana. Kufanya kazi kwa Bidii na kutofarikiana, Maendeleo yanahitaji mshikamano wa pamoja katika kusonga Mbele.

Share this post :

Chapisha Maoni


Get This:Techkgp

PAGE VIEWERS

About Me

Blog Archive

Blog za rafiki zangu

Get This:Techkgp
3D Live Statistics
 
Support : The Bantu | Mufandish | Mufandish Inc
Copyright © 2011. MUFANDISH NEWS - All Rights Reserved
Template Created by Mufandish Inc Published by Mufandish Mufandish
Proudly powered by Blogger