Machapisho

KAMUSI YA KINGEREZA KISWAHILI

Kamusi ya Kingereza - Kiswahili na Kinyume chake

ONA UFUNDI WA JUAN MATA, JE? UTAIKOMBOA MAN U??????

 Cheki hiyo then toa maoniiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii

ANNE WAITHERA ALIYEKUWA MWANDISHI WA SHIRIKA LA HABARI LA BBC AFARIKI DUNIA

Picha
Shirika la habari la BBC limempoteza kiungo wake muhimu  Ann alikuwa anafanya kazi na BBC katika ofisi za Nairobi na amekuwa akiugua Saratani ya Ubongo kwa karibu miaka miwili. Kabla ya kujiunga na BBC Ann alifanya kazi na shirika la habari la Nation Media Group nchini Kenya na Citizen TV. Ann alikuwa na umri wa miaka 39.Ann aliwahi kuwa ripota wa BBC mjini Addis Ababa Ethiopia. Waandishi wenza wa Ann BBC wameelezea watakavyomkumbuka Ann katika enzi zake alipokuwa anafanya kazi nao. Razvan Scortea mmoja wa wakuu wa BBC amesema : "Nimeshtushwa sana na kifo cha Ann. Alikuwa mtu mzuri , mwerevu mpenda watu na mwenye matumaini kwa kila jambo. Mungu ambariki.'' Mkuu wa BBC Afrika Solomon Mugera ameelezea kuwa ni jambo la kuhuzunisha sana kumpoteza Ann. ''Nimehuzinika sana. Anne alikuwa mwandishi mahiri . Kila nilipomtembelea nilivutiwa sana na matumaini ya Ann kupona. Hata katika mkesha wa krismasi, nilipozungumza na Ann alikuwa mcheshi sana. Nakumbu...

SERIKALI ZA CHINA NA JAPAN ZAING'ANG'ANIA AFRIKA

Picha
  China na Japan zimeanza kukosoana kuhusu sera zao barani Afrika huku kila nchi ikiahidi kuongeza kiwango cha cha msaada kwa bara hilo kila mwaka. Japan imesema kuwa China inawahonga viongozi wa Afrika kwa kuwapa zawadi za kifahari. Wakati huohuo, China inaituhumu Japan kwa kufanya urafiki na viongozi wa Afrika ili waunge mkono azma yake ya kutaka kuwa mwanachama wa kudumu wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa. Kiongozi wa Japan, Shinzo Abe anazuru mataifa matatu ya Afrika, ikiwa ziara yake ya kwanza barani humo na pia ni ziara ya kwanza ya waziri mkuu wa Japan katika kipindi cha miaka minane. Bwana Abe anatarajiwa kuahidi msaada wa dola bilioni 14 na pia kutia saini mikataba ya kibiashara nchini Ethiopia, Ivory Coast na Msumbiji. China kwa upande wake imekuwa ikisifu Afrika kama mahala pa ukelezaji na imeahidi kuongeza msaada wake kwa bara hilo mara dufu hadi dola bil...

NIPE NGONO NIKUPE SAMAKI

Picha
  Wanawake wa Kenya wanaofanya biashara ya kuuza Samaki katika ufuo wa ziwa Victoria mjini Kisumu Magharibi mwa nchi, wanajaribu kukomesha tabia ya kujihusisha na wavuvi kingono ili wapewe Samaki bila malipo. Tabia hii imelaumiwa pakubwa kwa kuchochea ongezeko la maambukizi ya HIV. Wakati wanawake hao wanapokubali kuwa na uhusiano wa kingono na wavuvi wanaume, basi hilo huwa kama hakikisho la kupata Samaki wa kuuza kwa kipindi kirefu. Biashara hii inayojulikana na wenyeji kama 'Jaboya', ambapo mwanamke anafanya Ngono na wavuvi ili apate Samaki wa kuuza, imelaumiwa pakubwa kwa kueneza maradhi ya Ukimwi miongoni mwa watu wanaoishi katika maeneo ya Ziwa Victoria. Sasa wanawake katika eneo hilo wamezindua kampeni inayolenga kukomesha biashara hiyo. Mradi uliozinduliwa na taasisi ya utafiti wa mazingira ya Victoria, umeanza kuwapa wanawake hao maboti yao ili waweze kufanya...

NI TAMU SANA LAKINI MADHARA YAKE.....

Picha
   HII NI TAMU SANA LAKINI MADHARA YAKE NI MAKUBWA Kikundi cha wanaharakati nchini Uingereza kimeanza juhudi za kutaka makampuni ya vyakula na vinywaji vya kuhifadhiwa kwenye chupa na mikebe kama Soda kupunguza kiwango cha sukari katika bidhaa zao. Hii ni sehemu ya kampeini ya kutaka kukabiliana na tatizo la kiafya la unene kupita kiasi pamoja na ugonjwa wa kisukari nchini humo. Kauli mbiu yao ni kuchukua hatua dhidi ya kiwango cha sukari kwenye chakula . Kikundi hiki kimeanzishwa na wanaharakati walioanzisha harakati za kushurutisha makampuni kupunguza kiwango cha Chumvi katika vyakula vinavyohifadhiwa kwenye mikebe tangu mwaka 1990. Wanaharakati hawa wanataka kuwajulisha watu kujizuia na vyakula vyenye sukari nyingi na kushurutisha wenye makampuni kupunguza sukari katika vyakula hivyo. Wanaamini kwamba makampuni yanaweza kupunguza bidhaa h...

MAELFU WAMZIKA ARIEL SHARON

Picha
  Maelfu ya watu nchini Israel wamekuwa wakitoa heshima zao za mwisho kwa hayati Ariel Sharon kabla ya mazishi yake hii leo. Jeneza la Sharon liliwekwa nje ya majengo ya bunge mjini Jerusalem jana Jumapili huku waombolezaji wakimiminika kumtolea heshima za mwisho kabla ya maziko. Sharon alifariki akiwa na umri wa miaka 85 baada ya kuwa hali mahututi kwa miaka 8, akitumia mashine kupumua Atafanyiwa ibada maalum ya kitaifa leo kabla ya kuzikwa karibu na shamba lake eneo la Sderot. Waisreli pamoja na viongozi wa dunia, wametoa heshima zao za mwisho , lakini wale ambao wanaweza kusema hawajaguswa sana na kifo cha Sharon ni wapalestina. Mwili wa Sharon ulifikishwa katika bunge la taifa Jumapili ambapo watu waliruhusiwa kuutizama siku nzima. Maombi yalifanywa huku bendera zikipepea nusu mlingoti. Watu waliendelea ku...