NI TAMU SANA LAKINI MADHARA YAKE.....

 
 HII NI TAMU SANA LAKINI MADHARA YAKE NI MAKUBWA

Kikundi cha wanaharakati nchini Uingereza kimeanza juhudi za kutaka makampuni ya vyakula na vinywaji vya kuhifadhiwa kwenye chupa na mikebe kama Soda kupunguza kiwango cha sukari katika bidhaa zao.
Hii ni sehemu ya kampeini ya kutaka kukabiliana na tatizo la kiafya la unene kupita kiasi pamoja na ugonjwa wa kisukari nchini humo.




Kauli mbiu yao ni kuchukua hatua dhidi ya kiwango cha sukari kwenye chakula .

Kikundi hiki kimeanzishwa na wanaharakati walioanzisha harakati za kushurutisha makampuni kupunguza kiwango cha Chumvi katika vyakula vinavyohifadhiwa kwenye mikebe tangu mwaka 1990.
Wanaharakati hawa wanataka kuwajulisha watu kujizuia na vyakula vyenye sukari nyingi na kushurutisha wenye makampuni kupunguza sukari katika vyakula hivyo.

Wanaamini kwamba makampuni yanaweza kupunguza bidhaa hiyo kwa asilimia 20 au 30 katika miaka mitano ijayo. Aidha wanaharakati wanataka kuiwekea malengo sekta ya chakula kupunguza kiwango cha sukari hatua kwa hatua kiasi cha wateja kukosa kutambua tofauti yoyote katika ladha ya vyakula hivyo.
Sukari ni bidhaa ambayo hutumiwa sana katika vyakula vingi ikiwemo, mikate, soda, vyakula vya mkebe na katika vyakula vingine ambavyo hata havihitaji sukari.  Na ndio maana sio jambo la kushangaza kuwa soda moja ya mkebe ina vijiko saba vya sukari. Maji, Yoghurt na vyakula vingine ambavyo hata havihitaji kuwa na sukari vinawekwa sukari








Share this post :

Chapisha Maoni


Get This:Techkgp

PAGE VIEWERS

About Me

Blog Archive

Blog za rafiki zangu

Get This:Techkgp
3D Live Statistics
 
Support : The Bantu | Mufandish | Mufandish Inc
Copyright © 2011. MUFANDISH NEWS - All Rights Reserved
Template Created by Mufandish Inc Published by Mufandish Mufandish
Proudly powered by Blogger