MAELFU WAMZIKA ARIEL SHARON


 
Maelfu ya watu nchini Israel wamekuwa wakitoa heshima zao za mwisho kwa hayati Ariel Sharon kabla ya mazishi yake hii leo.

Jeneza la Sharon liliwekwa nje ya majengo ya bunge mjini Jerusalem jana Jumapili huku waombolezaji wakimiminika kumtolea heshima za mwisho kabla ya maziko.
Sharon alifariki akiwa na umri wa miaka 85 baada ya kuwa hali mahututi kwa miaka 8, akitumia mashine kupumua
Atafanyiwa ibada maalum ya kitaifa leo kabla ya kuzikwa karibu na shamba lake eneo la Sderot.
Waisreli pamoja na viongozi wa dunia, wametoa heshima zao za mwisho , lakini wale ambao wanaweza kusema hawajaguswa sana na kifo cha Sharon ni wapalestina.
Mwili wa Sharon ulifikishwa katika bunge la taifa Jumapili ambapo watu waliruhusiwa kuutizama siku nzima.
Maombi yalifanywa huku bendera zikipepea nusu mlingoti.
Watu waliendelea kumiminika nje ya jengo hilo wengine wakiwasha mishumaa katika hatua ya kumuenzi Sharon.
Wageni mashuhuri wanatarajiwa kuhudhuria ibada maalum ya Ariel katika bunge la taifa wakiwemo makamu wa Rais wa Marekani Joe Biden, waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov, mjumbe maalum wa Mashariki ya kati Tony Blair, na waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier.
Sharon anakumbukwa na wengi kwa siasa zake na harakati zake dhidi ya wapalestina wakati akiwa mwanajeshi. Aliidhinisha ujenzi wa makazi ya walowezi katika eneo la Palestina na pia baadaye tume ya uchunguzi ilimpata na hatia ya kukosa kuzuia mauaji ya wapalestina yaliyofanywa na wakristo wa Phalangist baada ya Iisrael kuvamia Lebanon.
Share this post :

Chapisha Maoni


Get This:Techkgp

PAGE VIEWERS

About Me

Blog Archive

Blog za rafiki zangu

Get This:Techkgp
3D Live Statistics
 
Support : The Bantu | Mufandish | Mufandish Inc
Copyright © 2011. MUFANDISH NEWS - All Rights Reserved
Template Created by Mufandish Inc Published by Mufandish Mufandish
Proudly powered by Blogger