MATOKEO YA KIDATO CHA NNE YA MWAKA 2012/2013 YATARAJIWA KUTANGAZWA MNAMO WIKI HII PAMOJA NA MATOKEO YA KIDATO CHA SITA BAADA YA KUONGEZEKA IDADI YA UFAULU KUTOKA 23% HADI 25%

Idadi ya ufaulu wa watahiniwa wa mwaka 2012/13 imeongezeka kutoka asilimia 23% hadi 25%  na imesemwa kuwa matokwe hayo yatatolewa mnamo wiki hii pamoja na matokeo ya kidato cha sita ambayo yamecheleweshwa kutoka kutoka na yale yaliyozuka juu ya ubadilishwaji wa matokeo ya kidato cha nne. habari hii inapatikana katika gazeti la mwananchi.
Habari ambazo gazeti hili imezipata zinasema matokeo hayo ambayo yamewezesha kiwango cha ufaulu kupanda na kufikia asilimia kati ya 54 na 57, huenda yakatangazwa wiki hii pamoja na yale ya kidato cha sita ambayo pia yamechelewa kutangazwa.

Chanzo cha habari kutoka Necta kimesema matokeo hayo mapya yanaonyesha kuwa, ufaulu wa kuanzia daraja la kwanza hadi la nne umeongezeka kutoka asilimia 34.5 kwa matokeo yaliyotangazwa awali na huenda yakafikia asilimia 57. Hii inamaanisha kwamba watahiniwa wapatao 82,000 ambao awali walikuwa wamepata sifuri katika matokeo ya awali sasa wamepanda na kupata madaraja ya ufaulu katika matokeo mapya.

Kwa matokeo hayo, watahiniwa wa mwaka 2012 watakuwa wamefanya vizuri kuliko wa mwaka 2011, ambao watahiniwa 225,126 sawa na asilimia 53.37 ya 349,390 waliofanya mtihani huo walifaulu.

Msemaji wa Necta, John Nchimbi alisema upangaji wa matokeo hayo ulikuwa bado unaendelea. “Ninachojua kwa sasa ni kuwa mchakato unaendelea na matokeo yatatangazwa mapema tu ili watoto waweze kujiunga na shule mapema,” alisema Nchimbi.

Pia alisema usahihishaji wa mitihani ya kidato cha sita umekamilika.

Matokeo ya awali

Matokeo ya awali yaliyotangazwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa yalionesha kuwa kati ya watahiniwa 367,756 waliofanya mtihani wa kidato cha nne mwaka jana, waliokuwa wamefaulu kwa daraja la kwanza mpaka la tatu walikuwa 126,847 ni sawa na asilimia 6.4. Waliopata daraja la nne walikuwa ni 103,327 ni sawa na asilimia 28.1. N ukweli ni kwamba matokeo haya hayakuwaridhisha wengi kwani ni matokeo ambayo hayakuwahi kutokea ukilinganisha na miaka ya nyuma iliyopita.




Katika matokeo hayo, watahiniwa 240,909 sawa na asilimia 65.5 walipata sifuri, hesabu ambayo imebadilika katika matokeo mapya ambayo yanaonyesha kuwa sasa waliopata daraja hilo ni 158,100 ambayo ni asilimia 43.

Hata hivyo, habari kutoka Necta zinasema kuwa licha ya kuwezesha kuongezeka kwa waliofaulu, matumizi ya kanuni mpya ya kukokotoa matokeo hayo yalisababisha zaidi ya wanafunzi 2,500 kushuka ufaulu ikilinganishwa na awali.

Maofisa mbalimbali wa Necta pamoja na wale wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na taasisi zake, walikutana mwishoni mwa wiki iliyopita kukubaliana masuala mbalimbali juu ya matokeo hayo pamoja na suala la matokeo ya wanafunzi hao 2,500 kabla ya kutangazwa wiki hii.

“Baada ya wajumbe kujadili suala lile, busara ilibidi itumike kwa hiyo hakuna mwanafunzi ambaye alama yake itashuka, kwa kawaida isingewezekana mtoto ambaye matokeo yalitoka akiwa amefaulu leo umwambie ameshuka,” kilieleza chanzo chetu.

Matokeo ya awali ndiyo chimbuko la kupitiwa upya baada ya wadau kuyalalamikia na kumlazimisha Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kuunda tume ya kuyachunguza Februari 23, mwaka huu.

Kabla ya tume hiyo kuhitimisha shughuli zake, ilitoa taarifa ya awali ambayo ilipendekeza kufutwa kwa matokeo hayo kwa maelezo kwamba Necta ilitumia kanuni mpya ya kukokotoa matokeo bila kushauriana na wadau.

Serikali ilitoa taarifa bungeni kwamba imeamua kufuta matokeo ya 2012 na kuamuru yapangwe upya kwa kufuata madaraja yaliyotumika mwaka 2011.





Share this post :

Chapisha Maoni


Get This:Techkgp

PAGE VIEWERS

About Me

Blog Archive

Blog za rafiki zangu

Get This:Techkgp
3D Live Statistics
 
Support : The Bantu | Mufandish | Mufandish Inc
Copyright © 2011. MUFANDISH NEWS - All Rights Reserved
Template Created by Mufandish Inc Published by Mufandish Mufandish
Proudly powered by Blogger