"Mzee Nelson Mandela yuko hospitalini
na hali yake bado si yenyekuridhisha.''
Rais mstaafu wa Afrika Kusini Nelson
Mandela, angali katika hali mbaya ingawa imeweza kudhibitiwa. Mandela amelazwa
katika hospitali moja mjini Pretoria. Maombi yakekuwa yakifanywa makanisani
kote nchini Afrika Kusini kumuombea Mandela ambaye anatibiwa kwa ugonjwa wa
mapafu.
Bwana Mandela, mwenye umri wa miaka
94, alipelekwa hospitalini mapema Jumamosi , ikiwa ni mara ya tatu kulazwa
hospitalini mwaka huu. Kwa mujibu wa duru za urais, Mandela
amekuwa akiugua kwa muda mjini Johannesburg baada ya kukumbwa tena na ugonjwa
wa mapafu. Alilazwa hospitalini baada ya hali
yake kuwa mbaya zaidi mnamo Jumamosi. Kwa mujibu wa taarifa za urais, Rais
President Jacob Zuma, amerejelea wito wake kwa watu nchini Afrika Kusini
kumuombea Madiba wakati huu anapougua.
Lakini mwandishi wa BBC mjini
Pretoria, Karen Allen, anasema kuwa kuna matumaini madogo kuwa Mandela
aliyeongoza vita dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi, huenda kupona. Anasema kuwa wengi walipata matumani
baada ya bintiye Mandela Zindzi, kusema kuwa babake yuko salama na kuwa
anaendelea kupata nafuu. Mkewe Mandela Graca Machel,
alifutilia mbali, ziara yake mjini London Jumamosi ili kuwa kando ya mumewe. Mandela alikuwa Rais wa Afrika
Kusini kati ya mwaka 1994 hadi 1999. Alifungwa jela miaka 27 na
anaaminika kuwahi kuugua ugonjwa wa mapafu alipokuwa akifanyishwa kazi ngumu
katika machimbo ya mawe akiwa jela.
Chapisha Maoni