LANA:MWANAMKE AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA MITANO JELA BAADA YA KUMTUPA MTOTO WAKE CHOONI

Mwanamke mmoja mkazi wa Manga A Jijini Mbeya amehukumiwa kifungo cha miaka
 5 jela kwa kosa la kutupa mtoto wake chooni.
Tukio hilo lilitokea Juni 14, Mwaka huu katika eneo hilo baada ya watoto waliokuwa wakicheza 
kugundua kuwepo kwa Mtoto katika choo cha shimo.
 
Mtuhumiwa baada ya kukamatwa amekiri kutenda kosa hilo na kwamba alifanya hivyo baada ya mzazi mwenzie kumkataa.
Ameongeza kuwa amelazimika kutupa katika choo cha jirani kwa sababu ni cha shimo 
tofauti na chao ambacho asingeweza kutupa mtoto huyo.
  
Rukia Haruna (31)  akitolewa nje  na Askari wa Jeshi la Polisi akitolewa nje
 ya  Mahakama kwenda Gerezani kutumikia kifungo cha miaka 5 Jela  
 
Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Archiles Mulisa mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Mbeya, Zabibu Mpangula, amemtaja Mtuhumiwa kuwa ni Rukia Haruna (31) mkazi wa Manga A Jijini Mbeya na kwamba kosa lake ni kinyume cha kifungu  218 kifungu kidogo cha 35 sura ya 16 ya mwaka 2002.

Share this post :

Chapisha Maoni


Get This:Techkgp

PAGE VIEWERS

About Me

Blog Archive

Blog za rafiki zangu

Get This:Techkgp
3D Live Statistics
 
Support : The Bantu | Mufandish | Mufandish Inc
Copyright © 2011. MUFANDISH NEWS - All Rights Reserved
Template Created by Mufandish Inc Published by Mufandish Mufandish
Proudly powered by Blogger