Wanawake wa Kenya wanaofanya biashara ya kuuza Samaki katika ufuo wa ziwa Victoria mjini Kisumu Magharibi mwa nchi, wanajaribu kukomesha tabia ya kujihusisha na wavuvi kingono ili wapewe Samaki bila malipo. Tabia hii imelaumiwa pakubwa kwa kuchochea ongezeko la maambukizi ya HIV. Wakati wanawake hao wanapokubali kuwa na uhusiano wa kingono na wavuvi wanaume, basi hilo huwa kama hakikisho la kupata Samaki wa kuuza kwa kipindi kirefu. Biashara hii inayojulikana na wenyeji kama 'Jaboya', ambapo mwanamke anafanya Ngono na wavuvi ili apate Samaki wa kuuza, imelaumiwa pakubwa kwa kueneza maradhi ya Ukimwi miongoni mwa watu wanaoishi katika maeneo ya Ziwa Victoria. Sasa wanawake katika eneo hilo wamezindua kampeni inayolenga kukomesha biashara hiyo. Mradi uliozinduliwa na taasisi ya utafiti wa mazingira ya Victoria, umeanza kuwapa wanawake hao maboti yao ili waweze kufanya...