UGANDA YAANZA VIZURI CHAN



 


Timu ya Taifa ya Uganda The Cranes ambayo ni miongoni mwa kutoka Afrika Mashariki jumapili iliwafurahisha mashabiki wake baada ya kuishikisha adabu Burkina Faso kwa jumla ya magoli 2 -1 katika mechi ya kundi B ya michuano Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani CHAN.
Magoli ya Uganda yalifungwa na Mshambuliaji Junior Yunus Sentamu ambaye alikuwa ndiye mchezo bora katika mechi hiyo.
Mechi hiyo iliamsha furaha ya mashabiki wa Uganda ambao walishangilia hata nje ya uwanja huku wakiisifu timu yao kwamba imeonyesha kiwango cha hali ya juu na inaweza kufika mbali katika mashindano hayo.
Mechi nyingine ya kundi B Zimbabwe ilitoka sare ya kutokufungana na Moroco. Jumanne Ghana walitarajiwa kumenyana na Congo Braziville huku Libya nao walitarajiwa kupepetena vikali na Ethiopia katika mechi nyingine za kundi C.
Share this post :

Chapisha Maoni


Get This:Techkgp

PAGE VIEWERS

About Me

Blog Archive

Blog za rafiki zangu

Get This:Techkgp
3D Live Statistics
 
Support : The Bantu | Mufandish | Mufandish Inc
Copyright © 2011. MUFANDISH NEWS - All Rights Reserved
Template Created by Mufandish Inc Published by Mufandish Mufandish
Proudly powered by Blogger