IPO HAJA YA KUMSAIDIA BI MWANAIDI VUAI SALEH ALIYEUNGUA KWA MAJI YA MOTO

 Bi Mwanaid Vuai Saleh akiwa ameathirika kiasi hicho kama anavyoonekanav pichani akiwa katika hospitali ya Jeshi Bububu Unguja akiendelea na Matibabu yake akisubiri misaada ya Wasamaria wema ili kupata kusafirishwa nje ya nchi kupata matibabu zaidi ili kurudisha hali yake kiafya.
Kwa  sasa amepata baraka zote kutoka Ofisi ya Mufti Zanzibar kupata missada kama inavyosomeka hapo chini. 

Kumradhini kwa kuweka picha hii ya Bi Mwanaid Vuai Saleh, kwa maadili ya habari haifai.

Aliyepata ajali hiyo ya  kuanguka wakati akiwa katika kazi zake za nyumbani na kuanguka katika sufuria la maji ya moto baada ya kuona kizunguzungu na kuangukia humo na kumuathiri kiasi hicho na kwa sasa amelazwa katika Hospitali ya Jeshi Bububu akipata matibabu ya majaraha hayo.
Bi Mwanaid Vuai ni Mkazi wa Shehia ya Chumbini Wilaya ya Mjini Unguja 
Anaomba msaada wa Fedha ili kusafirishwa nje ya Nchi kupelekwa India kwa matibabu  zaidi 
Kwa kila Mwananchi atakayepata fursa ya kumsaidi Bi Mwanaid Vuai, ili kupata matibabu, anaombwa kuwasiliana na Mdau wa Blog hii, kwa Namba  0777424152.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA ZA KIAFYA ZA KITUNGUU MAJI KATIKA MWILI WA MWANADAMU

UFAHAMU MMEA WA MLONGE NA NAMNA UNAVYOFANYA KAZI NDANI YA MWILI WA MWANADAMU