Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana
akiwahutubia wananchi wa jimbo la Urambo,katika Mkutano wa hadhara uliofanyika
kwenye viwanja vya Mwananchi Skwea mjini Urambo,mkoani Tabora.
Ndugu
Kinana akiwa ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi,Siasa na Uenezi,Nape Nnaye yuko
katika ziara ya mikoa mitatu ya Tabora,Singida na Manyara,ya kuimarisha uhai wa
chama,kukagua miradi mbalimbali ya maenedeleo inayotekelezwa na kusimamiwa na
Serikali ya CCM,na pia kusikiliza matatizo ya wananchi na kuyapatia ufumbuzi.
Katika
mkutano huo wa hadhara uliowakutanisha Wana Urambo kwa wingi,Kinana pia
alisimikwa Uchifu wa kabila la Wanyamwezi.Kubwa zaidi Kinana pia alikabidhi
piki piki 16 na baiskeli 95 kwa ajili ya watendaji wa chama cha CCM katika kata
na matawi,zilizotolewa na Wabunge Mh,Samwel Sitta wa jimbo la Urambo Mashariki
na Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Tabora,Mh.Magreth Sitta.
Baadhi
ya Wananchi wa Mji wa Urambo wakiwa wamefurika kwenye uwanja wa
Mwananchi Skwea,wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana kwenye
mkutano wa hadhara,uliofanyika Wilayani Urambo,Kinana akiwa ameambatana
na Katibu wa NEC Itikadi,Siasa na Uenezi,Nape Nnaye yuko mkoani Tabora
kwa ziara ya siku 11,za kuimarisha uhai wa chama,kuhimiza utekelezaji wa
Ilani ya CCM,na kusikiliza matatizo mbalimbali ya wananchi.
Wabunge
Mh,Samwel Sitta wa jimbo la Urambo Mashariki akiwahutubia wakazi wa Mji
wa Urambo, na kulia ni Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Tabora,Mh.Magreth
Sitta.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akikabidhi moja ya piki piki 16 kwa mmoja wa makatibu wa Kata,Bwa.Baraka ambazo zilizotolewa na Wabunge Mh,Samwel Sitta wa jimbo la Urambo Mashariki na Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Tabora,Mh.Magreth Sitta.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akikabidhi baiskeli kwa mmoja wa viongozi wa
chama hicho,Bi Fatma Ulaya mjini Urambo katika mkutano wa hadhara
Katibu wa NEC Itikadi,Siasa na Uenezi,Nape Nnaye akiwahutubia Wananchi wa Mji wa Urambo kwenye uwanja wa Mwananchi Skwea
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwa ameketishwa kwenye Kigoda akifanyiwa
tambiko mara baada ya kusimikwa Uchifu wa kabila la Wanyamwezi.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman akikabidhiwa silaha ya jadi Mkuki,na
mmoja wa wazee wa Kinyamwezi mara baada ya kusimikwa Uchifu wa kabila
hilo mbele ya umati mkubwa wa wakazi wa mji wa Urambo.
Chapisha Maoni