MAADHIMISHO YA KITAIFA YA WIKI YA ELIMU TANZANIA YAFANYIKA DODOMA

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Ghalib Bilal akiwa na moja ya tuzo zilizotolewa kwa walimu wa Shule zilizofanya vizuri katika Elimu 2013 wakati wa kilele cha wiki ya Elimu, Kushoto ni Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi Dkt Shukuru Kawambwa na Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Rehema Nchimbi.
Makamu wa Rais Dkt Ghalib Bilal akimpatia cheti Mwanafunzi Nelson Athon wa shule ya sekondari ya Kizilego iliyopo mkoani Bukoba baada ya kufanya vizuri mwaka jana.
  MATUKIO YA PICHA

 Mkuu wa Shule ya Sekondari ya wasichana ya Msalato ya Dodoma akiwa ameshika mfano wa hundi ya Milion 3 zilizotolewa na Selikari kama motisha kwa shule hiyo kupandisha kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi kwa mwaka 2012/ 13 motisha hiyo imetolewa kwa jumla ya shule 14 za sekondari na 46 za msingi nchini, wakati wa kilele cha maadhimisho ya wiki ya Elimu.
 Mshairi wa  sanaa ya lugha katika Muziki Mrisho  Mpoto na Banana Zoro wakitoa Burudani katika kilele cha wiki ya Elimu iliyofanyika Kitaifa Mkoani Dodoma.
 Wanafunzi shule za msingi na Sekondari wakiwa majukwaani na mabango yenye ujumbe mbalimbali wakati wa kilele cha maadhimisho ya wiki ya Elimu yaliyofanyika Dodoma.
 Wanafunzi wa shule mbambali za msingi na Sekondari wakiwa wamezagaakutembelea mabanda ya maonyesho ya wadau wa Elimu katika siku ya mwisho ya maadhimisho ya wiki ya Elimu kabla ya kufungwa.
Wanafunzi na walimu ambao shule zao zimefanya vizuri wakiwa katika jukwaa maarumu walipokuwa wakisubili tuzo na zawadi mbalimbali zilizotolewa na Makamu wa Rais Dkt Ghalib Bilal wakati wa kilele cha wiki ya Elimu iliyohitimishwa jumamos Mei 10, 2014 iliyofanyika kitaifa Dodoma.

Share this post :

Chapisha Maoni


Get This:Techkgp

PAGE VIEWERS

About Me

Blog Archive

Blog za rafiki zangu

Get This:Techkgp
3D Live Statistics
 
Support : The Bantu | Mufandish | Mufandish Inc
Copyright © 2011. MUFANDISH NEWS - All Rights Reserved
Template Created by Mufandish Inc Published by Mufandish Mufandish
Proudly powered by Blogger