RAIA MIAMBILI (200) KUSHITAKIWA NCHINI MISRI

 
Mwendesha mashtaka mkuu nchini Misri

Mwendesha mashtaka nchini Misri amewafungulia mashtaka watu 200 wanaodaiwa kuwa wanachama wa kundi moja la waislamu wenye itikadi kali kutokana na misururu ya mashambulizi dhidi ya vitengo vya usalama.

Hatahivyo hakuna terehe iliotolewa ya kuanza kusikizwa kwa kesi dhidi ya wanachama hao wa kundi la Ansar Bet Al maqdis.
Takriban wanacham 100 wa kundi hilo ambao kesi zao ziko tayari kuanza hawajulikani waliko. Kundi hilo limekiri kutekeleza mashambulizi kadhaa , mengi yakifanywa baada ya kuondolewa madarakani kwa aliyekuwa rais wa taifa hilo Mohammed Morsi. Maafisa wamelishtumu kundi la Muslim Brotherhood kwa kupanga ghasia hizo madai ambayo yamepingwa na kundi hilo.
Share this post :

Chapisha Maoni


Get This:Techkgp

PAGE VIEWERS

About Me

Blog Archive

Blog za rafiki zangu

Get This:Techkgp
3D Live Statistics
 
Support : The Bantu | Mufandish | Mufandish Inc
Copyright © 2011. MUFANDISH NEWS - All Rights Reserved
Template Created by Mufandish Inc Published by Mufandish Mufandish
Proudly powered by Blogger